Mpango huu, uliozinduliwa na Uongozi wa Masuala ya Kidini wa Msikiti Mkuu wa Makka (Masjid al Haram) na Msikiti wa Mtume (Al Masjid An Nabawi), unalenga kuwahudumia mahujaji na wageni kupitia rasilimali mbalimbali za kielimu na kiroho zinazotolewa kwa lugha tofauti.
Kituo hiki kinatoa nakala za Qur'ani Tukufu zilizo tarjumiwa kwa lugha mbalimbali, pamoja na vijitabu vinavyohusu misingi ya imani ya Kiislamu, ibada za Hija na Umrah, misingi ya mitazamo ya wastani katika Uislamu, na mada zinazohusiana na usalama wa kimawazo na kiroho.
Kituo hiki cha uelimishaji ni cha kwanza miongoni mwa zaidi ya vituo 100 vya elimu na maarifa kwa lugha mbalimbali vinavyotarajiwa kufunguliwa katika viwanja vya Msikiti Mkuu wakati wa msimu wa Hija wa mwaka 1446 Hijria.
Juhudi hizi ni sehemu ya mpango wa kiutendaji wa Uongozi wa Msikiti kwa ajili ya kuboresha vipengele vya kitamaduni, kiroho, na kielimu vya ibada ya Hija
Uzinduzi huu unakuja wakati ambapo mahujaji kutoka pembe zote za dunia wameanza kuwasili kushiriki ibada ya Hija mwaka huu.
3493049