IQNA

Mkusanyaji wa Saudia ana Misahafu Adimu 214

21:57 - March 04, 2025
Habari ID: 3480305
IQNA – Raia mmoja wa Saudia ametumia miaka 40 kukusanya Misahafu adimu, akikusanya jumla ya nakala 214, kila moja ikiwa na historia yake ya kipekee.

Hussain Ourfali, mkusanyaji, alizungumza na televisheni ya Al Arabiya, akielezea uhusiano wake wa kina na Qur’ani Tukufu.

"Kila moja ya Misahafu hii ina hadithi maalum," alisema. "Nimekusanya msahafu wa kwanza uliyochapishwa kwa mashine duniani, ambao una kurasa 60."

Ourfali pia anamiliki maandishi yaliyoandikwa na mmoja wa waandishi maarufu zaidi wa kaligrafia katika ulimwengu wa Kiislamu. "Msahafu huu una zaidi ya miaka 1,200," alibainisha.

Alipoulizwa kuhusu motisha yake, Ourfali alisema shauku yake inatokana na hamu ya kuhudumia Qur’ani na kuhifadhi historia yake. "Nina hamu kubwa ya kukusanya nakala hizi adimu," aliongeza.

3492146

Habari zinazohusiana
Kishikizo: misahafu kale
captcha