IQNA

22:30 - August 25, 2021
Habari ID: 3474226
TEHRAN (IQNA)- Idara ya Masuala ya Kidini Katika Ofisi ya Rais wa Uturuki (Diyanet) imetangaza kuwa karibu watoto milioni 2 walifaulu katika kozi za kuhifadhi Quran zilizofanyika kote nchini.

Kwa mujibu wa taarifa kozi hizo ziliandaliwa kwa wiki sita, kutoka Julai 5 hadi Agosti 20.

Wataalamu 110 wa kiume na wa kike walisimamia kozi hizo, zilizoandaliwa katika misikiti 61,000 na vituo vya elimu 13,000 kote Uturuki

Programu za Qur'ani za mwaka huu zilifanyika kwa ushiriki wa wavulana milioni 1.03 na wasichana 874,000.

Misikiti na vituo vya elimu vya Uturuki viliandaa kozi za kibinafsi kwa watoto wa miaka 4 hadi 9.

Watoto kutoka umri wa miaka 10 hadi 15 walihudhuria kozi za kibinafsi na za kawaida na wale wenye umri wa miaka 16 hadi 22 walichukua kozi za mtandaoni.

Licha ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani, kozi hizo zilijumuisha masomo kuhusu mafundisho ya dini, maadili ya Kiislamu na sayansi ya Kiislamu.

Washiriki walienziwa katika hafla ya kufunga programu hiyo katika Msikiti wa Hagia Sophia huko Istanbul.

3992751

Kishikizo: uturuki ، diyanet ، qurani tukufu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: