IQNA

17:35 - February 05, 2021
Habari ID: 3473623
TEHRAN (IQNA)- Msikiti unaoaminika kuwa mdogo zaidi duniani unaojulikana kama Masjid Mir Mahmood Shah au Jinn ki Masjid huko Hyderbad nchini India unahitaji ukarabati wa dharura.

Msikiti huo uliojengwa karne ya 16 Miladia na Waislamu wa Twariqa una ukubwa wa futi -mraba 110 na uko katika mlima unaojulikana kama Mir Mahmodd ki Pahadi. Msikiti huo uko pembizoni bwawa kubwa la Amir Alam.

Katika uwanja wa msikiti pia kuna kaburi la Syed Shah Imaad Uddin Mohammed Mahmood Al Husaini, maarufu kama Mir Mahmood ki Pahadi. Inadokezwa kuwa ni watu 12 tu wanaoweza kuswali ndani ya msikiti huo.

Usanifu majengo wa msikiti huo ni ule wa mbinu ya Qutb Shahi na sasa unahitaji ukarabati. Njia ya kuelekea katika msikiti huo ulio mlimani pia inahitaji ukarabati.

Pamoja na hayo kuna misikitimingine inayotajwa kuwa midogo zaidi duniani. Wa kwanza ni ule ulioko Bhopal nchini India na mwingine katika mji wa  Naberezhnye Chelny nchini Russia lakini kwa mujibu wa vipimo, Jinn ki Masjid unabakia kuwa mdogo zaidi duniani.

3473890

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: