IQNA

India yapunguza chuki dhidi ya Waislamu baada ya malalamiko ya kimataifa

12:10 - April 30, 2020
Habari ID: 3472719
TEHRAN (IQNA) – Chama tawala nchini India, Bharatiya Janata (BJP), kimetoa wito wa umoja na maelewano ya kidini baada ya malalamiko ya kimataifa kufuatia ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu nchini humo.

Hatua ya BJP kulekgeza msimao imekuja baada ya viongozi wa Waislamu duniani kupinga vikali madai ya serikali ya India kuwa mjumuiko mmoja au Ijtimai ya kundi la kuhubiri Uislamu ya Tablighi Jamaa ndio chanzo cha asilimia 30 ya maambukizi ya corona (COVID-19) nchini India.

Siku ya Jumapili mkuu wa jumuiya ya Rashtriya Swayamsevak Sangh (RSS), ambayo ni mrengo wa wanamgambo wa BJP, alitoa wito kwa watu wote kuungana katika kukabiliana kwa pamoja na corona.

Mkuu  huyo wa RSS Mohan Bhagwat ambaye anatajwa kuwa kinara ya Wahindu wenye misimamo mikali amesema watu wote wa India ni familia moja. "Sote ni kitu kimoja, ni makosa kuilaumuu jamii nzima kutokana na makossa ya wachache."

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi naye amewatumia Waislamu salamu kwa mnasaba wa kuanza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kusema: "Tunaomba Mwezi Huu Mtukufu ulete neema ya ukarimu, maelewano na kuhurumiana. Tunaomba tupate uchini mkubwa dhidi ya COVID-19 ili dunia iwe na afya."

Ijumaa iliyopita Waziri wa Mambo ya Nje wa India Subrahmanyam Jaishankar aliwapigia simu mawaziri wenzake katika nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi na kuwahakikisha kuwa Waislamu India hawatabaguliwa.

3471302

captcha