IQNA

Muongozo wa Ramadhani
11:37 - April 22, 2021
News ID: 3473839
TEHRAN (IQNA) – Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni fursa kwa Waislamu kustawisha mtindo wa Kiislamu maishani.

Hayo yamesemwa na Hujjatul Islam Muhammad Muhsin Radmard, mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW katika nchi za Marekani na Canada.

"Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unatupa fursa ya kuonyesha wengine mtindo wa Kiislamu katika maisha ili wasiokuwa Waislamu wawezi kuona taswira halisi ya Uislamu." Amesema kwa tabia na mwenendo mwema maishani, Waislamu wanaweza kuuhubiri Uislamu bila kutamka neno.

Amesongeza kuwa Waislamu wanapaswa kurejea katika ustaarabu halisi wa Uislamu ili kila anayemattazama Muislamu apate taswira halisi ya Uislamu.

Halikadhalika Hujjatul Islam Muhammad Muhsin Radmard amesema Waislamu wametakiwa kuhakikisha kuwa kuna usawa katika Mwezi wa Ramadhani na pia wanapaswa kuonyesha udugu na kujitolea katika mwezi huu.

Aidha amesema katika mwezi huu Mwislamu anapata uzoefu wa njaa ili kwa njia hiyo aweze kuhusi hali waliyonayo wale wasiojiweza na kwa njia hiyo muumini anapata motisha ya kuwasiadia wengine. Mwanazuoni huyo ameongeza kuwa, Infaq au kutoka kwa njia ya Mwenyezi Mungu ni kati ya mambo yaliyopewa umuhimu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Nukta nyingine ambayo ameashiria katika mwezi huu ni kuwaheshimu wengine wawe ni wazee au vijana.

Kwa ujumla huu ni mwezi wa kujiboresha mja nafasi yake na pia kuiboresha jamii kwa ujumla.

3474526

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: