IQNA

Filamu ya Matukio ya kweli ya ''Katika Magwanda ya Askari" yazinduliwa Tanzania

12:45 - June 24, 2021
Habari ID: 3474037
TEHRAN (IQNA)- Filamu ya matukio ya kweli inayojulikana kama "'Katika Magwanda ya Askari" iliyotarjumiwa kwa lugha ya Kiswahili imezinduliwa hivi karibuni nchini Tanzania.

Filamu hiyo inahusu simulizi maalumu ya Ayatullahil- Udhmaa Sayyid Ali Khamenei katika medani za vita vya kulazimishwa vya Iraq dhidi ya Iran hadi katika jaribio la mauwaji la 27/7/1981.

Kwa mujibu wa taarifa ya mwandishi wa IQNA, mwambata wa utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Dar es Salaam Murtadha Pirani amepokea nakala ya filamu hiyo hivi karibuni kutoka Salum Bendera ambaye ameitarjumu kwa lugha ya Kiswahili.

Filamu ya matukio ya kweli imeandaliwa katika Taasisi ya Utafiti wa Kiutamaduni ya Mapinduzi ya Kiislamu Ofisi ya kuhifadhi na kueneza athari za Ayatullahil - Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Unaweza kuitazama filamu hiyo katika anuani ifuatayo ya YouTube

https://www.youtube.com/watch?v=aQZHUNItSN4

3979428

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :