IQNA

Spika wa Bunge la Iran

Vikwazo vya kidhalimu dhidi ya Iran viondolewe kwa maptano adilifu

19:24 - December 01, 2021
Habari ID: 3474625
TEHRAN (IQNA)- Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, amesema haki za taifa la Iran zitarejeshwa tu iwapo kutafikiwa mapatano maziri na adilifu ambayo yatapalekea vikwazo kuondolewa.

Akizungumza leo bungeni, Mohammad Baqer Qalibaf, amesema ana uhakika kuwa kufuatia jitihada ambazo zimetekelezwa katika uga wa sera za kigeni, haki za taifa la Iran zitarejeshwa kwa kufikiwa mapatano mazuri ambayo yataondoa mzigo wa vikwazo katika mabega ya wananchi.

Akizungumza katika kikao hicho cha wazi cha bunge ambacho kilihudhuriwa na Rais Ibrahim Raisi, Qalibaf amesema zimepita siku zaidi ya 100 tangu serikali ya awamu ya 13 ianze kazi zake na hakuna shaka kuwa rais amefanya kazi kubwa.

Qalibaf ameashiria jitihada za serikali za kukabiliana na janga la COVID-19 na kusema idadi ya vifo vinavyotokana na COVID-19 imepungua kutoka 700 kwa siku hadi 70 kwa siku katika kipindi cha siku 70.

Aidha amesema uhusiano wa serikali ya awamu ya 13 na bunge la 11 ni mzuri kwa ajili ya mustakbali wa nchi. Qalibaf amesema bunge linataraji serikali itachukua hatua kukabiliana na matatizo kama vile ukosefu wa ajira na nyumba na pia ongezeko la bei za bidhaa.

Spika Qalibaf amesema bunge litashirikiana na serikali ili kufanikisa mikakati ya kutatua matatizo ya wananchi.

4017648

captcha