IQNA

Mwanazuoni: Qur'ani Tukufu ni muujiza wa daima

20:54 - December 29, 2021
Habari ID: 3474740
TEHRAN (IQNA)- Mwanazuoni mwandamizi nchini Iran amesema Qur'ani Tukufu ni muujiza wa kudumu.

Akizungumza mjini Tehran Jumanne wakati wa kufunga  Tamasha la 36 la Qur'ani na Itrat katika Wizara ya Sayansi, Utafiti naTeknolojia, Hujjatul Islam wal Muslimin Kadhim Sidiqquie amesema tokea kuteremshwa kwake, Qur'ani Tukufu imetoa changamoto kwa wengine kuwasilisha sura kama zake na hakuna aliyeweza kufanya hivyo.

Amesema ni miujiza michache tu ya Qur'ani iliyoweza kugunduulika hadi sasa na kwamba badi kuna nukta nyingi sana za siri za Qur'ani ambazo bado mwanadamu hajaweza kuzibaini.

Amesema Qur'ani Tukufu ina maelezo ya kisayansi kama vile kuhsu embryolojia, mime n.k ambayo wanadamu walikuwa hawayajui wakati wa kuteremshwa kwake.

Hujjatul Islam Siddiquie ameashiria aya ya pili ya Sura al Baqara isemayo:" Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu." Na kuongeza kuwa, Qur'ani Tukufu ni kitabu cha kumuongoza mwanadamu ili aweze kufukia ukamilifu.

4024361

captcha