IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni akiba isiyomalizika na inapaswa kutumiwa ipasavyo

15:49 - February 04, 2022
Habari ID: 3474887
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo mjini Tehran amesema: "Mapinduzi ya Kiislamu sawa na matukio ya Ashura na Ghadir ni akiba isiyomalizika na inapaswa kutumiwa ipasavyo."

Hujjatul Islam wal Muslimin Kadhim Siddiquie, Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran ametoa salamu za kheri na fanaka kwa mnasaba wa kuwadia mwaka wa 43 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa: "Wananchi wa Iran waliopata ushindi wanapaswa kufanya sherehe za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu kila mwaka sambamba na kuvifahamisha vizazi vijavyo kuhusu fikra ya kina ya mapinduzi haya ya kihistoria."

Hujjatul Islam wal Muslimin Kadhim Siddiquie amesema Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran hayana mfano wake duniani na kuongeza kuwa, " Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalikuwa na taathira kote duniani na yaliweza kubadilisha historia sambamba na kuleta mageuzi katika uhusiano wa kimataifa." Ameongeza kuwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalikuwa tukio la kuandaa matayarisho ya ulimwengu kukubali uadilifu na usawa.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ameendelea kusema kuwa, mhimili wa Mapinduzi ya Kiislamu ulikuwa ni kiongozi mwandamapinduzi na faqihi mkubwa ambaye ni Imam Khomeini- Mwenyezi Mungu Amrehemu.

Amesema kuwa Imam Khomeini MA alifanikiwa kuleta mabadiliko miongoni mwa wananchi waliokuwa wamepotoshwa na hivyo wakaweza kufuata miongozo yake.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amebaini kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu yaliyoongozwa na Imam Khomeini (MA) yalikuwa ni yenye kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya mwanadamu na ambayo yaliweka msingi mwema wa kumcha Mwenyezi Mungu.

4033680

Habari zinazohusiana
captcha