Imam Hassan Mujtaba AS ni mjukuu wa Mtume SAW na mtoto wa kwanza wa Imam Ali bin Abu Taleb na Bibi Fatima Zahra SA. Alizaliwa katika siku ya kumi na tano ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka wa 625, aliishi mika saba wakati wa maisha ya Mtume Muhammad SAW na baada ya kifo cha mtukufu huyo, alikuwa na baba yake katika matukio hayo.. Baada ya kuuawa shahidi Imam Ali AS, Hassan Mojtaba AS alikuwa mrithi wake kama Imamu wa umma..
Hassan bin Ali alifundishwa na Mtume SAW na Imam Ali ibn Abi Talib AS, na wakati wa maisha yake, alizingatia masuala ya jamii. Alikuwa na mtazamo wa kina kuhusu maarifa ya Mwenyezi Mungu kwa misingi ya elimu ya aliyopata kutoka kwa babu yake, Mtume Mtufufu SAW.
Kwa msingi huo alikuwa na mtazamo wa kina kuhusu dunia na matukio yake na hivyo aliweza kuzitazama shida na misukosuko ya maisha kwa mtazamo huo. Kwa mtazamo kama huo matatizo hayaweza kuleta msukosuko katika moyo ya mwandamu au kumsimamisha katika harakati zake bali hutazamwa kama fursa ya ya kuimarisha nafsi.
Kwa maneno mengine, wakati mtu anataka kumsifu Mwenyezi Mungu kwa sifa zake anasema : "Shukrani zote ni kwa Mungu tu ambaye hana mipaka. Fikra ya mwanadamu bado haijaweza kumdiriki kikamilifu. Yeye si wa jambo fulani, na si kwa kitu fulani, na si kwa kitu, na sio kutoka katika ulimwengu.
Aliyoanza Mwenyezi Mungu hayakuwa na historia, huyu yu ndiye Mungu wako ambaye ni Bwana wangu (Kutoka kitabu cha Tawhidi cha Sheikh Sadough) Sheikh Sadough amechunguza kwa kina suala la Tawhidi na mjadala kuhusu asili ya Mungu.