IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Libya yaanza tena

22:59 - May 29, 2022
Habari ID: 3475312
TEHRAN (IQNA) - Baada ya miaka kadhaa ya kusimamishwa kwa sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, mashindano ya kimataifa ya Quran ya Libya yatafanyika tena mwaka huu.

Kwa mujibu wa tangazao la Kituo cha Quran na Sunnah cha Wakfu na Wizara ya Masuala ya Kiisilamu, Duruy  ya 10 la  mashidano hayo itaanza katika jiji la Benghazi mnamo Juni 11,

Mashidano yatakuwa katika kategoroa za qiraa na kuhifadhi Qur’ani Tukufu imesema taarifa hiyo.

Halikadhalika taarifa hiyo imesema  kuanza tena Mashidano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu Libya baada kusitishwa miaka kadhaa, ni habari njema kwa wasomi wa Qur’ani kote duniani.

Wale walio tayari kushiriki katika mashindano wanaweza kuwasiliana na kituo hicho kupitia anwani ya baruapepe au email ambayo ni  oqaflibya@gmail.com au kupitia nambari ya WhatsApp +218925791706.

Libya imekuwa katika msukosuko tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoungwa mkono na muugano wa kijeshi wa NATO unaongozwa na Marekani mnamo 2011. Mapigano hayo yalipelekea kuuawa mtawala wa muda mrefu wa nchi hiyo Muammar Gaddafi na tokea wakati huo nchi hiyo imekuwa katika mgogoro ingawa hivi sasa hakuna mapigano lakini mivutano ya kisiasa ingali inaendelea.

4060413

captcha