IQNA

Libya kuchapisha tena Mus’haf wa Taifa

15:15 - December 03, 2025
Habari ID: 3481610
IQNA – Mwenyekiti wa Kamati ya Qur’ani ya Jumuiya ya Ulinganiaji wa Kiislamu nchini Libya ametangaza kuchapishwa upya kwa Qur’ani ya taifa (Mus’haf wa Taifa wa Libya) kwa ajili ya kusambazwa bure kwa wananchi.

Al-Tahami Al-Zaytouni amesema nakala za bure za toleo la kwanza la Mus’haf wa Taifa wa Libya, toleo la 16, zimekwisha, kwa mujibu wa Libya Press.

Ameongeza kuwa seti ya toleo hili ilitengwa mahsusi kwa usambazaji wa bure, na nakala zote zimeshaisha. Kutokana na mahitaji makubwa, uchapishaji wa Qur’ani hii utaendelea.

Mus’haf wa Taifa wa Libya umeandikwa kwa riwaya ya Imam Qalun kutoka kwa Imam Nafi’ Al-Madani, na kwa mtindo wa Imam Abu Omar Al-Dani, mtindo ambao umekuwa maarufu katika shule na madrassah (maktab) za Qur’ani nchini Libya.

Mus’haf wa Taifa wa Libya ulianza kuchapishwa mwaka 1982 na umekuwa rejeleo kuu kwa vizazi vingi katika kuhifadhi Qur’ani Tukufu.

Libya ni nchi yenye Waislamu wengi kaskazini mwa Afrika, na inakadiriwa kuwa na zaidi ya wahifadhi milioni moja wa Qur’ani.

Nchi hiyo imekuwa katika hali ya machafuko tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosaidiwa na NATO mwaka 2011 vilipoondoa na kumuua dikteta wa muda mrefu Muammar Gaddafi.

Katika miaka ya hivi karibuni, Libya imegawanyika kati ya serikali ya umoja wa kitaifa mjini Tripoli na utawala wa mashariki.

3495599
Kishikizo: msahafu libya
captcha