IQNA

Harakati za Qur'ani

Kituo cha Qur’ani chazinduliwa huko Sirte nchini Libya kwa michango ya umma

19:29 - March 09, 2024
Habari ID: 3478474
IQNA - Kituo cha kuhifadhi Qur'ani na kufundisha sayansi ya Qur'ani kimezinduliwa huko Sirte, mji ulio kaskazini mwa Libya.

Kituo hicho kimeanzishwa katika Msikiti wa Badr kwa mchango wa kifedha wa watu wa jiji hilo.

Ilizinduliwa katika hafla ya Alhamisi, iliyohudhuriwa na meya Sirte na maafisa kadhaa wa kidini, tovuti ya habari ya AL-Wasat iliripoti.

Wakati wa hafla hiyo, idadi ya wanafunzi wakuu wa Qur’ani wa jiji hilo pia walitunukiwa kwa ufaulu wao.

Sirte ni mji wa pwani ya Mediterania ulioko kilomita 450 mashariki mwa mji mkuu wa Libya wa Tripoli.

Libya ni nchi yenye Waislamu wengi Kaskazini mwa Afrika ambayo ina zaidi ya watu milioni waliohifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu.

Nchi hiyo imekuwa katika machafuko tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoungwa mkono na muungano wa kijeshi wa kibeberu za Magharibi, NATO, mwaka 2011 na kupelekea kupinduliwa na kuuawa dikteta mkongwe Muammar Gaddafi.

Libya katika miaka ya hivi karibuni imegawanyika kati ya serikali ya umoja wa kitaifa huko Tripoli na utawala ulioko mashariki.

Shughuli za Qur'ani ni maarufu sana nchini humo licha ya miaka mingi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na mapigano kati ya makundi hasimu.

3487480

Kishikizo: libya qurani tukufu
captcha