IQNA

Haki za Watoto

Hali ya utumikishaji watoto barani Afrika

11:05 - June 13, 2022
Habari ID: 3475371
TEHRAN (IQNA)- Tarehe12 Juni, kama ilivyo ada ya kila mwaka, jumuiya ya kimataifa inaungana na kusema hapana kwa ajira ya watoto. Licha ya kupungua kwa idadi ya watoto wanaofanya kazi katika miongo miwili iliyopita, maendeleo kuelekeza kutokomeza ajira kwa watoto yalitatizwa katika kipindi cha mwaka 2016 hadi 2020.

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinasema hivi sasa wasichana na wavulana milioni 160 wanafanya kazi. Na wengine kati yao wakiwa na umri wa miaka mitano. 

Vita dhidi ya umaskini 

Katika Siku hii ya kimataifa dhidi ya Ajira kwa Watoto, Umoja wa Mataifa na wadau wake wanajielekeza kwenye uwekezaji zaidi katika ulinzi wa kijamii na mifumo inayowalinda watoto dhidi ya vitendo hivyo. 

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mifumo ya ulinzi wa kijamii inayotolewa na serikali za ulimwengu ni muhimu katika kupambana na umaskini kwa kutokomeza na kuzuia utumikishwaji wa watoto. 

Ulinzi wa kijamii ni haki ya binadamu na sera yenye nguvu ya kuzuia familia kutoajiri watoto wakati wa shida. 

Mwaka 2020, kwa mfano, wakati na kabla ya janga la ugonjwa wa Covid-19, ni asilimia 46.9 tu ya idadi ya watu ulimwenguni ililindwa ipasavyo na angalau faida moja ya ufadhili kutoka serikali. Na asilimia 53.1 iliyobaki, jumla ya watu bilioni 4.1, hawakuwa na usaidizi au ufadhili wa kifedha kutoka serikali. 

Misukosuko ya kiuchumi, masomo ya nyumbani 

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ulinzi kwa watoto ni mdogo zaidi. Karibu robo tatu ya watoto, au watoto bilioni 1.5 duniani, hawana usaidizi wowote wa kijamii. 

Kuadhimisha siku hii ya kimataifa dhidi ya ajira kwa watoto,  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi Duniani, ILO, na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto,UNICEF, wanapaswa kuzingatia ripoti iliyowasilishwa katika mkutano wa 5 wa Kimataifa kuhusu Ajira ya Watoto, uliofanyika mwezi Mei mwaka huu, ukiwa na takwimu za tafiti zilizofanywa tangu mwaka 2010. 

Katika tafiti hizo hali ya ulinzi wa kijamii zinachambuliwa na jinsi familia zinavyokabiliana na misukosuko ya kiuchumi na kiafya huku zikipigania ajira ya watoto na kukuza elimu nyumbani. 

ILO inaeleza kwamba watoto wengi wana aina za kazi za kulipwa au zisizolipwa duniani kote ambazo hazina madhara kwao lakini wakati mtoto ni mdogo sana kufanya kazi au kufanya shughuli ambazo ni hatari kwake au zinaweza kuhatarisha ukuaji wake wa kimwili, kiakili, kijamii au kielimu, basi hiyo ni ajira ya watoto. 

Amerika na Afrika 

Katika nchi zinazoendelea, zaidi ya mtoto mmoja kati ya wanne wenye umri wa kati ya miaka 5 na 17 ni mwathirika wa utumikishwaji wa watoto, ambao unachukuliwa kuwa hatari kwa afya na maendeleo yao. 

Bara la Afrika ndilo eneo lenye idadi kubwa ya matukio ya watoto katika hali hii. Kuna watoto asilimia 20 au milioni 72 wanaofanya kazi. Asia na Pasifiki zinaonekana katika nafasi ya pili na 7 ya watoto wote na watoti  milioni 62, kwa maneno namna zote, wakiwa katika hali hiyo ya utumikishwaji. 

Kwa pamoja, maeneo ya Asia-Pasifiki na Afrika yana takriban visa tisa kati ya 10 vya utumikishwaji wa watoto duniani. Namba nyingine zinatoka Amerika yenye milioni 11, Ulaya na Asia ya Kati na milioni 6, na Mataifa ya Kiarabu yenye milioni 1. 

Kwa upande wa matukio, asilimia 5 ya watoto wanaofanya kazi wako Amerika, asilimia 4 Ulaya na Asia ya Kati na asilimia 3 katika nchi za Kiarabu. 

Ingawa asilimia ya watoto kazini ni kubwa zaidi katika nchi za kipato cha chini, idadi hiyo ni kubwa zaidi katika mataifa yenye kipato cha kati. Asilimia 9 ya watoto wote katika nchi zenye kipato cha kati chini wanatumikishwa na asilimia 7 ya watoto wote katika mataifa yenye kipato cha kati. 

4063389

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :