IQNA

Historia ya Uislamu

Msikiti ulio karibu na Madina unaosimulia kisa cha Vita vya Uhud

15:00 - July 25, 2022
Habari ID: 3475537
TEHRAN (IQNA) – Kuna msikiti karibu na mji mtakatifu wa Madina unaoitwa Msikiti wa Sayed Al-Shuhada ambao ni eneo muhimu katika historia ya Kiislamu.

Msikitu huu unasimulia kisa cha Vita vya Uhud, vilivyotokea katika mwaka wa tatu wa Hijria.

Pia uko karibu na makaburi ya mashahidi 70 ambao walikuwa masahaba wa Mtume Muhammad (SAW), yapata kilomita tatu kutoka eneo la  kaskazini wa Msikiti wa Mtume, Masjid Nabawi mjini Madina.

Ujenzi wa msikiti huo ulikamilika mwezi Aprili 2017 na una mtindo wa kipekee wa usanifu na una ukubwa wa mita za mraba 54,000 ambapo unaweza kubeba hadi waabudu 15,000.

Msikiti huo pia unaelekea upande wa Mlima Rumat, kilima kidogo kilichoko magharibi mwa Mlima Uhud.

Vyanzo vya kihistoria vinasema kwamba jeshi la kabila la Quraysh na washirika wake lilikwenda Madina kuwaua Waislamu na kulipiza kisasi kwa wale waliokufa katika Vita vya Badr, vilivyotokea mwaka wa pili wa Hijiria.

Waislamu walikabiliana nao, huku Mtume Muhammad (SAW) akiweka wapiga mishale kwenye Mlima Rumat. Aliwaamuru wapiga mishale kubaki kwenye vituo vyao hadi watakap;oamurishwa kuhama.

Washambuliaji walipoanza kukimbia, wapiga mishale walifikiri kwamba vita vimekwisha na kwamba walikuwa wameshinda. Walishuka mlimani, wakipuuza amri ya Mtukufu Mtume (SAW).

Kamanda wa washambuliaji, Khalid bin Al-Walid, ambaye alikuwa bado hajasilimu, aliwashangaza wapiga mishale waliokuwa wakishuka, akawaua, kisha akawashambulia Waislamu wengine.

Masahaba sabini wa Mtume waliuawa, akiwemo ami yake Hamzah bin Abdul-Muttalib. Walizikwa kwenye uwanja wa vita kwenye msingi wa Mlima Rumat.

Waislamu wanazuru makaburi yao hadi leo, kama Mtume Muhammad (SAW) alivyofanya siku moja. Waabudu pia hupanda mlimani kutazama eneo la vita.

 

A Mosque near Medina that Tells Story of Battle of Uhud

A Mosque near Medina that Tells Story of Battle of Uhud

3479828

captcha