IQNA

Maelfu ya wenyeji wahudhuria Mashindano ya 48 ya Kitaifa ya Qur'ani Sanandaj

15:54 - October 27, 2025
Habari ID: 3481425
IQNA – Kwa wastani, zaidi ya watu 5,000 kutoka mkoa wa Kordestan nchini Iran huhudhuria mashindano ya kitaifa ya Qur'an kila siku, kwa mujibu wa afisa mmoja.

Toleo la 48 la Mashindano ya Kitaifa ya Qur'an nchini Iran lilianza tarehe 18 Oktoba katika mji wa Sanandaj, na linatarajiwa kufungwa leo tarehe 27 Oktoba kwa hafla ya hitimisho itakayohudhuriwa na viongozi wa kitaifa, wa mikoa, na wa jamii.

Hujjatul-Islam Mohammad Karvand, mkuu wa Idara ya Waqfu na Masuala ya Hisani ya Kordestan, alisema: “Safari hii tumeshuhudia mwitikio wa kipekee kutoka kwa wananchi. Ukumbi mkuu na ukumbi wa pili walijaa kabisa, hata sehemu ya nje haikuwa na nafasi ya kuketi.”

Hujjatul-Islam Karvand aliongeza kuwa washiriki kutoka mikoa 31 wamekusanyika Sanandaj baada ya kufuzu katika hatua za mikoa.

Alifafanua kuwa hakutakuwa na tukio lolote katika jengo kuu asubuhi ya siku ya kufunga mashindano. Hafla ya kufunga imepangwa kuanza saa 12 jioni.

Pia alieleza kuwa washiriki bora katika kila kundi watatunukiwa zawadi. Katika baadhi ya vitengo, zawadi hutolewa hadi nafasi ya tano, na washindi wa juu wataendelea kushiriki mashindano ya kimataifa.

Alisisitiza tena kuwa “kwa wastani, zaidi ya watu 5,000 huingia kila siku katika kumbi na maeneo ya jirani ya mashindano na kushuhudia matukio.”

Karvand pia alieleza kuhusu utofauti wa kikabila na wa kieneo miongoni mwa waliohudhuria. Alibainisha kuwa watu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi walifika Kordestan, na kuwa wakazi wa Sanandaj na wilaya jirani walihudhuria wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni ya Kikurdi, hali iliyozidisha upekee wa kiroho na kitamaduni wa hafla hiyo.

3495166

Habari zinazohusiana
captcha