Hujjatul-Islam Sayyid Mehdi Khamoushi ametoa kauli hiyo katika hotuba yake ya wakati wa hafla kufunga Mashindano ya 48 ya Kitaifa ya Qur’ani Tukufu nchini Iran, iliyofanyika jioni ya Jumatatu katika mji wa Sanandaj, mkoa wa Kordestan.
Akizungumzia mafanikio ya mashindano ya Qur’ani yaliyofanyika kote nchini, amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inajivunia kuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa ya Qur’ani yanayofanyika kwa mfululizo zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu.
Alibainisha kuwa hata wakati wa vizuizi vya COVID-19, mashindano haya yaliendelea kwa njia ya mtandao na bendera ya Qur’ani haikuwekwa chini.
Amesisitiza kuwa mikusanyiko kwa ajili ya Qur’ani ni fursa ya kuongoza maisha kwa mwangaza wa Qur’ani na kuongeza kuwa, Iran inapaswa kuwa, kwa dhati, kitovu cha Qur’ani katika ulimwengu wa Kiislamu.
Aidha, alieleza kuwa Qur’ani Tukufu ni katiba ya maisha mema na mwongozo kwa jamii ya waumini, na hivyo jamii yoyote inayoiweka Qur’ani kuwa msingi wa maisha yake itachukua mkondo wa furaha na heshima.
Akigusia mapambano ya kudumu kati ya upande wa haki na upande wa batili katika historia, mkuu huyo wa Taasisi ya Wakfu amezungumza kuhusu matukio ya siku hizi katika ulimwengu wa Kiislamu, na kusema kuwa Madoka ya kiistikbari na kibeberu duniani hayatambui kitu kinachoitwa haki na hulazimisha mataifa kukubali batili.
“Hivi karibuni, afisa mmoja wa Marekani alisema: Ikiwa Iran itaachana na Mapinduzi ya Kiislamu, basi wako tayari kwa mazungumzo! Lakini taifa la Iran limejengwa kwa msingi wa Qur’ani na kamwe halitaachana na malengo yake ya kimungu.”
Ameongeza kuwa leo, kamera zote duniani zinarekodi jinai za Marekani na utawala wa Kizayuni huko Gaza, na maoni ya umma duniani yamegundua kuwa Marekani ndiyo chanzo kikuu cha dhulma dhidi ya watu wa Palestina.
“Katika mazingira kama haya, ni lazima tutambue ni ipi safu ya haki na ipi safu ya batili. Watu waumini wa Iran wamesimama katika safu ya haki na maadui wa Uislamu wamesimama katika safu ya batili.”
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, akirejelea Aya ya 18 ya Surah Al-Hashr, “Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kila nafsi itazame ilichokitanguliza kwa ajili ya kesho; na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye khabari na mnayoyatenda,” alisema kuwa Taqwa (kumcha Mungu) si tu kujiepusha na dhambi binafsi; bali ni uchaji wa kijamii, yaani kulinda imani na kutekeleza wajibu wa pamoja wa Ummah wa Kiislamu.
Alisema muumini anapaswa daima kujitathmini: je, yuko upande wa haki au wa batili?
🔹 Soma Zaidi:
Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani Iran: Washindi Watangazwa
Hujjatul-Islam Khamoushi pia amesisitiza umuhimu wa kujikurubisha na Mwenyezi Mungu, akisema, “Ulimwengu hauendeshwi kwa msingi wa maada na fizikia pekee; bali uongozi wa ulimwengu uko mikononi mwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Mtu asiye na uhusiano na Mungu, ingawa anaonekana kuwa hai, kiuhalisia ni mfu anayetembea.”
Aliongeza kuwa uhai wa kweli unapatikana pale roho ya mtu inapoungana na Mwenyezi Mungu. “Yeyote anayesahau kumkumbuka Mungu katika maisha yake, kwa hakika amekufa kiroho.”
Mwanazuoni huyo amesisitiza umuhimu wa kusoma Qur’ani kila siku kama jambo la lazima kwa kila muumini ili roho ya mwanadamu iishi kwa neno la Mwenyezi Mungu.
Alihitimisha hotuba yake kwa kuwashukuru waandaaji wa mashindano hayo na watu wa Sanandaj ambao, kwa kuhudhuria kwao, walionesha mshikamano wa Kiislamu na ukaribu na Qur’ani Tukufu.
Washindi wa Mashindano ya 48 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu nchini Iran katika makundi mbalimbali walituzwa mwishoni mwa hafla hiyo.
4313234