IQNA

Mashindano ya Pili ya Kimataifa ya Usomaji na Kuhifadhi Qur'ani Tukufu Yafanyika Astana, Kazakhstan

7:17 - October 17, 2025
Habari ID: 3481374
IQNA – Tarehe 15 Oktoba, katika Msikiti Mkuu wa Astana, Kazakhstan, mashindano ya pili ya Kimataifa ya Usomaji na Kuhifadhi Qur'an Tukufu yamekamilika, yakileta pamoja washiriki 22 kutoka mataifa 21. Tukio hili limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Mambo ya Kiislamu ya Saudi Arabia na Mamlaka ya Kiroho ya Waislamu wa Kazakhstan.

Mashindano haya ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Jamhuri ya Kazakhstan na kumbukumbu ya miaka 35 tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Kiroho ya Waislamu wa Kazakhstan.

 Washiriki walikuwa kutoka katika mataifa mbalimbali ikiwemo Iran, Saudi Arabia, Bahrain, UAE, Misri, Palestina, Morocco, Algeria, Jordan, Türkiye, Malaysia, Pakistan, Kyrgyzstan, Azerbaijan, Indonesia, Tajikistan, Uzbekistan, Russia, Chechnya na Tatarstan.

Akizungumza katika ufunguzi, Mufti Mkuu wa Kazakhstan Sheikh Nauryzbai Kazhy Taganuly alisisitiza nafasi ya Qur'an ikatika jamii na maisha ya kifamilia:
"Mwaka huu tumeutangaza kuwa 'Mwaka wa Uislamu na Maadili ya Familia' kwa watumishi wa dini. Mashindano haya ya kimataifa ya Qur'ani ni miongoni mwa juhudi muhimu katika muktadha huo. Mtu anayetekeleza mafundisho ya Qur'ani hujali familia, huwakuza watoto kwa maadili, na humchukulia mwenzi wake kama amana kutoka kwa Mwenyezi Mungu.”

Miongoni mwa washiriki ni Hujjatul Seyyed Ali Hosseini kutoka Qom, Iran, aliyeteuliwa na Kituo cha Masuala ya Qur'an cha Shirika la Misaada na Wakfu la Iran

Mashindano haya yameendelea kwa siku mbili na kufikia kilele Alhamisi kwa hafla ya kufunga, ambapo Mufti Mkuu Sheikh Nuri-Zhubai Otebnuf ameungana na mawaziri, mabalozi, wasomi na viongozi wa dini kutoka mataifa shiriki.

Tukio hili linakusudia kuonyesha umuhimu wa Qur'an katika maisha ya Waislamu na kuimarisha mshikamano wa udugu wa Kiislamu duniani.

 

4310921

 

Habari zinazohusiana
captcha