IQNA

Fikra za Kiislamu

Sisitizo la Qur’ani Tukufu kuhusu kuepuka ujinga

20:07 - October 07, 2022
Habari ID: 3475893
TEHRAN (IQNA) – Jahl (ujinga) ni sifa isiyofaa kwa mwanadamu kwani sio tu kwamba inaleta madhara kwa mtu mwenyewe, bali pia inaweza kuwapoteza watu wengine au makundi ya watu.

Ndio maana kila mtu anapaswa kujitahidi kujiweka mbali na wajinga.

Neno Jahl kwa Kiarabu lina maana tofauti, ikiwa ni pamoja na ujinga, kutokuwa na ufahamu na ukosefu wa elimu na ufahamu.

Uislamu unawausia waumini waepuke Jahl, ukitaja madhara yake mbalimbali.

Qur’ani Tukufu inataja sababu tofauti za Jahl: “ Yusuf akasema: Ee Mola Mlezi wangu! Nastahabu kifungo kuliko haya anayo niitia. Na usipo niondoshea vitimbi vya wanawake mimi nitamili kwao, na nitakuwa katika wajinga.” (Sura Yusuf, Aya ya 33).

Kwa mujibu wa Nabii Yusuf (AS) katika aya hii, kutenda madhambi kunamfanya mtu kuwa mjinga. Nukta  nyingine kuhusu Jahl katika Sura hii ya Qurani: “Akasema: Je! Mmejua mliyo mfanyia Yusuf na nduguye mlipo kuwa wajinga?” (Sura Yusuf, Aya ya 89).

Jahl wakati fulani hutokana na matamanio ya kidunia na wakati mwingine kutokana na uzembe. Hata kama mtu ana ujuzi, ikiwa anapuuza matokeo ya tabia yake mbaya, kwa kweli ni mjinga.

Sababu nyingine ya ujinga ni tabia isiyofaa. Kwa mfano kuwadhihaki wengine inasemekana kuwa ni ishara ya kutojua.

“Na Musa alipo waambia watu wake: Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mchinje ng'ombe. Wakasema: Je! Unatufanyia mzaha? Akasema: Audhubil lahi! Najikinga kwa Mwenyezi Mungu nisiwe miongoni mwa wajinga. (Surah Al-Baqarah, Aya ya 67)

Jahl ni kitu kinachozuia ukuaji wa kiakili na kibinafsi wa mtu. Hiyo ni sababu nyingine kwa nini kuna mapendekezo mengi kuhusu kuepuka. Quran Tukufu inasema katika aya ya 6 ya Surah Al-Hujurat:

 Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda..

Kuwauliza wale wanaojua ni njia ya kujikinga na ujinga: “Nasi hatukuwatuma kabla yako ila watu wanaume tulio wapa Wahyi(Ufunuo). Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui." Surah An-Nahl, Aya ya 43)

captcha