IQNA

Fikra za Kiislamu

Mtazamo wa Uislamu kuhusu amali njema

16:39 - October 10, 2022
Habari ID: 3475908
TEHRAN (IQNA) – Kwa mujibu wa misingi ya mafundisho ya Kiislamu, ni matendo tu ambayo yanamweka mwanadamu kwenye njia ya uongofu ndiyo yatakayokubaliwa na Mwenyezi Mungu; na kwa hivyo amali njema huambatana na imani na nia njema.

Qur'ani Tukufu imetaja baadhi ya vigezo vya matendo na tabia ya mwanadamu na kwa msingi huo amali njema zilizofanyika kwa ikhlasi au nia njema ni kigezo cha msingi cha mwanadamu mwenye kufaulu.

Uislamu unaamini kwamba kila tendo linapaswa kutathminiwa kwa kuzingatia nia na motisha nyuma yake, na si kwa kuzingatia maslahi ya kimaada. Maadamu nia njema haiambatani na amali njema hatuwezi kukitaja kitendo  hicho kuwa ni "kizuri" au cha "haki".

Kwa mujibu wa kanuni za Kiislamu, thamani ya matendo ya kila mtu iko katika nia na sifa zake za kiroho na kiakili. Tendo jema ni lile lililoundwa na kufanywa kwa kuzingatia kanuni kama vile Kuamini Mungu na Siku ya Kiyama na pia kwa kuzingatia hisia na motisha nzuri.

Ndio maana Uislamu umeharamisha unafiki na unatazama vitendo visivyo na makusudio ya Mwenyezi Mungu kuwa ni vitendo visivyo na thamani hata kama vitendo hivi vina sura ya kuvutia. “Haiwi kuwa makafiri ndio waamirishe misikiti ya Mwenyezi Mungu, hali wanajishuhudishia wenyewe ukafiri. Hao ndio ambao vitendo vyao vimeharibika, na katika Moto watadumu.” (Sura At-Tawbah, aya ya 17)

Uislamu unawataka wanadamu kujiweka mbali na kitendo chochote kinachojumuisha hadaa, ria au kujionyesha udanganyifu.

Hii ni sehemu ya kitabu cha Seyyed Mohammad Baqir Sadr

captcha