IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu Ufaransa

Msomi: Chuki dhidi ya Uislamu ni sera ya kiserikali Ufaransa

13:56 - October 16, 2022
Habari ID: 3475936
TEHRAN (IQNA) - Msomi na mwanafikra wa Ufaransa amesema chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) haikomei kwa chama fulani bali ni sera ya serikali nchini Ufaransa.

Francois Burgat alikosoa tawala za Ufaransa kwa kuchochea moto wa chuki dhidi ya Uislamu nchini humo.
Alisema chuki hizo zimefika viwango vya hatari nchini Ufaransa na kwingineko barani Ulaya.
Hapo awali, chuki dhidi ya Uislamu ilihusiana zaidi na vikundi vya mrengo mkali wa kulia lakini leo hii serikali pia zimeingiza chuki hiyo katika sera rasmi, amebaini.
Burgat alisema serikali ya Ufaransa imevuka mipaka kwa hatua zake za chuki dhidi ya Uislamu, na kuongeza kuwa hatua zake zimewatatiza Waislamu wote nchini humo.
François Burgat, ni mwanasayansi wa siasa wa Ufaransa na ni mtafiti katika Kituo cha Kitaifa cha Utafiti wa Kisayansi cha Ufaransa.
Kuna Waislamu wapatao milioni 5.7 wanaoishi Ufaransa, idadi kubwa zaidi ya Waislamu katika nchi moja Ulaya Magharibi.
Serikali ya Ufaransa katika miaka ya hivi karibuni imefuata sera ya kuweka vikwazo juu ya uhuru wa Waislamu wa nchi hiyo. Hatua hizo zimedhoofisha haki za Waislamu katika nchi hiyo ya Ulaya.
Wanakabiliwa na aina tofauti za mapungufu, chuki na ubaguzi.
Hata misikiti haijahifadhiwa na hivi karibuni serikali imefunga baadhi ya maeneo ya ibada ya Waislamu kwa visingizio mbalimbali visivyo na msingi.

4092052

captcha