IQNA

Wanafunzi wanyimwa chakula Halal katika baadhi ya shule za Ufaransa

16:43 - October 24, 2022
Habari ID: 3475982
TEHRAN (IQNA) – Tatizo la chakula katika mikahawa ya shule nchini Ufaransa ni keri kubwa kwa wazazi wengi wa wanafunzi Waislamu.

Baadhi ya mameya wameamua kutotoa menyu mbadala ya chakula 'Halal' katika mikahawa ya shule wakitumia kisingizio kuwa mfumo wa utawala nchini humo ni wa kisekulari au usio wa kidini

Mfano ni katika eneo  Tassin-la-Demi-Lune, nje kidogo ya mji Lyon, ambapo tangu 2016 wakuu wa manispaa hiyo wameamua kwamba menyu moja tu itolewe kwa chakula cha shule.

Na wakati mlo pekee unaotolewa wakati mwingine unahusu nyama ya nguruwe, wanafunzi Waislamu wanaotaka chakula Halal kilichotayarishwa kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu au Mayahudi wanaotaka chaula 'Kosher' kilichotayarishwa kwa mujibu wa itikadi za Kiyahudi wana shida ya kupata chakula wakitakacho.

Ili kukabiliana na tatizo hili, baadhi ya mameya wamependekeza orodha ya walaji mboga pekee, wakitaja masuala ya mazingira.

Wakikabiliwa na ukosefu wa huruma wa mameya, wazazi katika shule ambapo nyama ya nguruwe ndiyo chaguo pekee walizindua ombi la mtandaoni la kudai menyu mbadala.

Watu kadhaa mashuhuri, akiwemo mwanahabari na mwanaharakati wa masuala ya wanawake Rokhaya Diallo, wameunga mkono ombi hilo na kuwahimiza wengine kulitia saini.

Nchini Ufaransa, Waislamu wanakabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara na kutengwa huku kukiwa na mjadala mkali kuhusu utambulisho wao.

3480977

Kishikizo: ufaransa waislamu halal
captcha