IQNA

Waislamu Ufaransa

Ufaransa yaanza mchakato wa kufunga msikiti mwingine

19:03 - September 29, 2022
Habari ID: 3475853
TEHRAN (IQNA) - Serikali ya Ufaransa inapanga kufunga msikiti mwingine, ikimtuhumu imamu wa masikiti husika kuwa na itikadi kali.

Wizara ya Mambo ya Ndani imeanza mchakato wa kufunga Msikiti wa Obernai katika eneo la Bas-Rhin, kulingana na TV ya BFM ya Ufaransa na Le Figaro.

Waziri wa Mambo ya Ndani Gerald Darmanin alisema kwenye Twitter kwamba "maeneo 23 ya ibada ya wanaotaka kujitenga" yamefungwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Aliongeza kuwa kufungwa kulikuja baada ya ombi la rais kupiga vita "harakati ya Kiislamu ya kutaka kujitenga."

Wizara hiyo inamtuhumu imamu wa Msikiti wa Obernai kwa kufanya shughuli za mahubiri ya itikadi kali, kuchukua mtazamo wa chuki dhidi ya jamii ya Ufaransa na kutoa maoni ya uchochezi dhidi ya maadili ya jamhuri hiyo.

Utawala wa Paris umekosolewa na jumuiya ya kimataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya haki za binadamu, hasa Umoja wa Mataifa, kwa sababu inalenga na kuwatenga, kuwakandamiza na kuwabagua Waislamu.

3480667

Kishikizo: ufaransa ، waislamu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha