IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

Sherehe ya kuwaenzi Wahifadhi Qur'ani Tukufu mjini Sharjah

15:19 - February 04, 2023
Habari ID: 3476510
TEHRAN (IQNA) – Wakfu wa Qur’ani Tukufu na Sunnah huko Sharjah, Umoja wa Falme za Kiarabu, uliandaa hafla ya kuwaenzi wenye kuhifadhi Qur’ani Tukufu.

Wakati wa hafla hiyo, iliyofanyika katika makao makuu ya taasisi hiyo, wavulana na wasichana 96 walipongezwa kwa mafanikio yao ya Qur'ani.

Walikuwa miongoni mwa watu 689 ambao waliweza kujifunza Qur’ani Tukufu nzima kwa moyo mnamo 2020 na 2021.

Wahifadhi 96 waliotunukiwa pia walikuwa wametimiza masharti yaliyowekwa na kamati maalum ya taasisi hiyo.

Sherehe hizo hufanyika kila mwaka na taasisi hiyo ili kuwahimiza wavulana na wasichana kuanza kuhifadhi Qur'ani Tukufu na kuimarisha ujuzi wao wa Qur'ani.

Qur’ani Tukufu ndio maandiko pekee ya kidini ambayo yanakaririwa na wafuasi wake.

Watu wasiohesabika katika kila umma wa Kiislamu wamehifadhi Qur’ani Tukufu tangu siku ya kwanza ilipoteremshwa.

Quran ina Juzuu (sehemu) 30, Sura 114 na aya 6,236.

 

4119422

Kishikizo: qurani tukufu ، sharjah
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha