IQNA

Turathi ya Kiislamu

Maonyesho ya Misahafu adimu huko Sharjah yanaendelea

20:31 - February 02, 2023
Habari ID: 3476503
TEHRAN (IQNA) – Jumba la Makumbusho ya Ustaarabu wa Kiislamu ya Sharjah nchini UAE yameongezwa muda hadi majira ya kiangazi.

Maonyesho hayo yana Misahafu (Nakala za Qur’ani Tukufu)  52  za karne ya 14 Miladia wakati wa ustaarabu wa Kiislamu kutoka China hadi Afrika Kaskazini na ni ni sehemu ya Mkusanyiko wa Misahafu wa Hamid Jafar.

Maonyesho hayo, yenye jina la "Maneno Matakatifu, Kaligrafia Isiyo na Wakati: a Kaligrafia ya Kipekee kutoka kwa Nakalaza Qur’ani za Hamid Jafar," yanaonyesha ufundi na undani wa vipande muhimu vya kaligrafia ya Kiislamu.

"Ninajivunia na kuheshimiwa kuonyesha Misahafu hii kutoka mkusanyiko wangu kwa mara ya kwanza katika Sharjah ninayoipenda ambayo nimeichukua kama nyumba yangu kwa zaidi ya nusu karne,” alisema Hamid Jafar, mwanzilishi na mwenyekiti wa Kundi la Makampuni la Crescent lenye makao yake Sharjah.

Misahafu 52 katika maonyesho inaonyesha ufundi na ustadi wa hali ya juu wakati wa kuandikwa.

3482325

captcha