IQNA

Shughuli za Qur'ani

Tarjuma za Qur'ani katika lugha tofauti Zinaonyeshwa kwenye Maonyesho ya Vitabu ya Sharjah

16:58 - November 06, 2022
Habari ID: 3476042
TEHRAN (IQNA) – Tarjuma za Qur’ani Tukufu katika lugha 76 ni miongoni mwa vitabu vilivyowasilishwa kwenye Maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Vitabu ya Sharjah.

Tarjuma hizo zimechapishwa katika Taasisi ya  Mfalme Fahd ya Uchapishaji wa Qur'ani Tukufu na zimeonyeshwa kwenye banda la Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudia.

Taasisi hiyo iko katika mji mtakatifu wa Madina na huchapisha takriban nakala milioni 10 za Qur'ani kila mwaka.

Pia huchapisha tarjuma za Qur'ani Tukufu katika lugha mbalimbali. Katika maonyesho hayo pia kuna aplikesheni za  Kiislamu, filamu za hali halisi, huduma za maktaba ya kielektroniki na vipeperushi kuhusu huduma za Hijja na Umrah.

Taasisi ya  Mfalme Fahd ya Uchapishaji wa Qur'ani Tukufu imetangaza kuwa itasambaza Misahafu 110,000 za katika maonyesho hayo.

Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Sharjah ynafanyika kwa muda wa siku 11 kuanzia  Novemba 2 hadi 13 huko Sharjah, Umoja Falme za Kiarabu.

"Eneza Neno" ndiyo kauli mbiu ya maonyesho ya mwaka huu.

 4097190

 
 
captcha