IQNA

Sharjah yafungua Tamasha la 26 la Sanaa za Kiislamu kwa Kauli mbiu ya “Taa”

20:26 - November 19, 2025
Habari ID: 3481540
IQNA – Sharjah imezindua Tamasha la 26 la Sanaa za Kiislamu, tukio la siku 70 linaloangazia urithi wa sanaa za Kiislamu kutoka duniani kote.

Tamasha hili limefunguliwa Jumatano kwa kauli mbiu ya “Taa”, likiandaliwa na Idara ya Masuala ya Utamaduni ya Sharjah na kufanyika katika Jumba la Sanaa la Sharjah.

Hafla hii iko chini ya usimamizi wa Sultan bin Muhammad Al Qasimi, mjumbe wa Baraza Kuu na mtawala wa Sharjah.

Mkurugenzi wa Tamasha la Sanaa za Kiislamu, Mohammed Ibrahim Al Qasir, amesema toleo la mwaka 2025 litajumuisha matukio 114 na kazi 473 za wasanii 170 kutoka nchi 24.

Amesema tamasha hili linaakisi maono ya mtawala wa Sharjah ya “kubadilisha sanaa kuwa ujumbe wa kitamaduni unaoeleza kiini cha ubinadamu”, na kuwa daraja la mawasiliano ya kiutamaduni baina ya mataifa.

Jumla ya maonyesho 52 yataandaliwa katika maeneo mbalimbali, yakiwemo Jumba la Sanaa la Sharjah, Jumba la Kaligrafia la Sharjah, Ukumbi wa Khorfakkan, na Jumuiya ya UAE ya Kaligrafia ya Kiarabu na Mapambo ya Kiislamu.

Ratiba ya tamasha inajumuisha maonyesho, warsha na makongamano kwa ushirikiano na taasisi 26 za Sharjah.

Tamasha la Sanaa za Kiislamu la Sharjah ni tukio la kimataifa lililoanzishwa mwaka 1998, lenye kujitolea kuonyesha upeo wa kiutamaduni na uzuri wa sanaa za Kiislamu, na kila mwaka huwasilisha mitindo mbalimbali ya ubunifu wa kisanaa.

Tamasha hili litaendelea hadi tarehe 31 Januari 2026, InshaAllah.

3495452

Kishikizo: sharjah qurani tukufu
captcha