IQNA

Wanazuoni Mashuhuri wa Ulimwengu wa Kiislamu/14

Kitabu cha Mwanachuoni wa Syria Mustafa Muslim juu ya Tafsiri ya Kimadhari ya Qur'ani Tukufu

21:02 - January 03, 2023
Habari ID: 3476352
TEHRAN (IQNA) – Kitabu kiitwacho ‘Mabahith fi Tafsir al-Madhuei’ (Majadiliano Kuhusu Tafsiri ya Kimadhari) ni mojawapo ya kazi kuu za mwanazuoni wa Syria Sheikh Mustafa Muslim kuhusu tafsiri ya Qur’ani.

Sheikh Mustafa Muslim (1940-2021) alikuwa mtu mashuhuri katika uwanja wa sayansi ya Qur'ani ambaye aliandika vitabu 90, zikiwemo ensaiklopidia za sayansi za Qur'ani Tukufu.

Mojawapo ya kazi zake kuu ni ‘Mabahith fi Tafsir al-Madhuei’ ambayo inaweza kuzingatiwa kama ensaiklopidia ya kwanza ya tafsiri ya Kurani ambayo inazingatia tafsiri ya Kimadhari au kimaudhui.

Ufafanuzi wa kimaudhui ni njia ya kujadili mada kwa kuzingatia aya za Qur'ani Tukufu ambamo mada hiyo imetajwa.

Kwa njia hii, mfasiri hukusanya aya mbalimbali zinazozungumzia somo la kawaida na kwa kuzichambua kwa pamoja ili kupata maoni ya Qur'an kuhusu suala hilo.

Ili kuandika kazi hiyo yenye juzuu 10, Sheikh Mustafa Muslim alisoma kwanza na kufundisha katika vyuo vikuu nadharia ya umoja wa maudhui katika Sura za Qur'ani Tukufu. Alipokuwa akifundisha katika Chuo Kikuu cha Sharjah mwaka 2004, alialika idadi kubwa ya wasomi wa sayansi ya Qur'ani kujadili nadharia hii.

Kulingana na nadharia hii, wanazuoni 30 kila mmoja walifanya kazi ya kufasiri Sura za Qur'ani Tukufu chini ya usimamizi wa Sheikh Mustafa Muslim.

Kitabu ambacho kilichapishwa katika juzuu kumi kinajumuisha tafsiri ya kimaudhui ya Sura zote za Qur'ani Tukufu

‘Mabahith fi Tafsir al-Madhuei’ kwanza inatoa mjadala kuhusu ufafanuzi, mzizi, maendeleo, aina na umuhimu wa tafsiri ya kimadhari ya Qur'ani Tukufu.. Waandishi wanasema njia hii inatokana na tafsiri ya Qur'an-kwa kutegemea Qur'ani ambayo ilikuja kuwa ya kawaida wakati wa Mtukufu Mtume (SAW, ingawa neno tafsiri ya kimaudhui lilitumika kwa mara ya kwanza katika karne ya 14 Hijria.

Kitabu kina utangulizi wa mwandishi na sura tano pamoja na hitimisho.

Sura ya kwanza, iliyopewa jina la ‘Tafsiri ya Kimaudhui’ inajadili maendeleo ya kihistoria ya sayansi ya ufasiri na hadhi ya ufasiri wa kimaudhui, umuhimu wake na aina zake.

Sura ya pili inajumuisha mbinu katika ufasiri wa kimaudhui na utafiti juu ya aya na Sura na uhusiano kati ya mada na aina nyinginezo za tafsiri.

Ya tatu inafafanua zaidi juu ya sayansi ya mahusiano (ambayo ni kuhusu njia ya Wahyi), umuhimu wake na kazi kuu katika uwanja huu.

Katika sura ya nne, msomaji anajifunza kuhusu mifano linganishi kuhusu mada moja katika Qur'ani Tukufu.

Sura ya tano inatoa mifano linganishi katika tafsiri ya kimaudhui kuhusu "maadili katika Surah Al-Kahf".

captcha