Alisoma aya ya 285 ya Surah Al-Baqarah, na Sura Al-Kawthar ya Kitabu kitukufu katika hafla hiyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema mwenye Kurehemu
“Mtume ameamini yaliyo teremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi wake, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake. Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na (Waumini) husema: Tumesikia na tumet'ii. Tunakutaka maghfira Mola Mlezi wetu! Na marejeo ni kwako. (Aya ya 285 ya Surah Al-Baqarah)
Naapa kwa alfajiri, Na kwa masiku kumi. Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja. Na kwa usiku unapo pita. Je! Hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili? (Al Fajr 1-5)
Hakika tumekupa kheri nyingi. Basi sali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi. Hakika anaye kuchukia ndiye aliye mpungufu. (Sura Al Kauthar)
Washindi wa tamasha hilo walitangazwa na kutunukiwa zawadi katika hafla ya kufunga hafla hiyo kuu ya sinema, ambayo ilifanyika kwenye Mnara wa Milad wa Tehran Jumamosi usiku.
Tamasha hilo hufanyika kila mwaka kwa mnasaba wa kumbukumbu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979 ya Iran.
Jafar Fardi alizaliwa mwaka 1981. Alianza kujifunza usomaji wa Qur'ani akiwa na umri wa miaka 8 kwa kuhudhuria vikao vya Qur'ani Tukufu vilivyokuwa vikifanywa na Mohammad Hossein Saeedian mjini Tehran.
Mnamo mwaka wa 2013, alishika nafasi ya kwanza katika Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani ya Iran na kufanikiwa kushinda nafasi ya kwanza katika Mashindano ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu.
4121738