IQNA

Shakhsia katika Qur'ani Tukufu /34

Ilyas; Nabii Aliye Hai Mbinguni

17:41 - March 11, 2023
Habari ID: 3476690
TEHRAN (IQNA) – Miongoni mwa Mitume wa Mwenyezi Mungu, wachache wanaaminika kuwa walibaki hai na hawakupata uzoefu wa kifo. Miongoni mwao ni Nabii Ilyas (Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake-AS-) ambaye alimuomba Mwenyezi Mungu amjaalie kifo baada ya watu wake kumuasi, lakini Mwenyezi Mungu alimlipa ujira mwema kwa kumuweka hai mbinguni.

Ilyas (AS) ni miongoni mwa Mitume wa Bani Isra’il. Alikuwa wa ukoo wa Harun (AS), ndugu yake Musa (AS). Aliteuliwa kuwa mjumbe wa Mwenyezi Mungu wakati wa utawala wa Ahabu, mfalme wa Bani Isra’il, katika mji wa Baalbek, katika Lebanoni ya sasa.

Ilyas (AS) alipewa jukumu la kuwalingania watu wake kwenye Tauhidi, kumtii Mwenyezi Mungu, na kuacha madhambi. Dhamira yake kuu ilikuwa ni kukabiliana na ibada ya masanamu ambayo ilikuwa imeenea na kuungwa mkono na wafalme wa Bani Isra’il.

Licha ya miaka mingi ya kuwaita watu wake kurejea kwa mafundishi ya Mwenyezi Mungu na kuacha ibada ya sanamu, walikataa kuukubali wito wake. Kisha akamwomba Mungu awaadhibu watu na wakatumbukia katika njaa.

Baada ya njaa kuchukua maisha ya watu wengi, watu walianza kujutia mwenendo wao na wakakubali mwaliko wa Ilyas (AS) wa kumwabudu Mwenyezi Mungu. Kisha nabii akaomba mvua inyeshe na ikaja, ikimaliza miaka ya njaa.

Hata hivyo, watu walisahau ahadi yao kwa Ilyas (AS) na wakarejea kwenye ibada ya masanamu. Akiwa amekabiliwa na hili, Ilyas (AS) aliomba kifo chake, lakini Mungu alimuweka hai na akampeleka mbinguni.

Inasemekana kwamba Ilays (AS) angeweza kuponya wagonjwa na kuwafufua wafu.

Jina lake limetajwa katika Quran mara mbili. Mara moja katika Surah Al-Maryam na halikadhalika katika Surah As-Saffat. Katika sura ya kwanza, ametajwa kuwa ni mtu mwema kando ya Zakariya (AS) na Yesu (AS) na katika nyingine kama nabii wa Mungu.

Pia ametajwa kama Al-e Yasin katika Surah As-Saffat. Baadhi ya wafasiri wa Qur'ani Tukufu ingawa, wanaamini kwamba Ilyas (AS) na Mtume Idris (AS) ni kitu kimoja kwa sababu baadhi ya sifa zao na hadithi za maisha yao zinafanana. Baadhi ya wengine wanaamini kwamba Ilyas (AS) na Khizr (AS) wana mambo mengi yanayofanana, kama vile ukweli kwamba wote wawili wamekwenda mbinguni wakiwa hai.

Katika Biblia, Ilyas (AS) anatajwa  kuwa Iliya. Hadithi nyingi kuhusu Ilyas (AS) katika Biblia pia zimetajwa katika vyanzo vya Kiislamu ingawa kuna tofauti kadhaa.

Ingawa wafasiri wengi wa Qur'ani Tukufu wanasema Ilyas (AS) yu hai mbinguni, wachache wanaamini kwamba alikufa na kuzikwa mahali panapowezekana kuwa Iran au Iraq.

captcha