IQNA

Ayatullah Jafar Sobhani

Mwanadamu ana kiu ya mafundisho ya Qur’ani zaidi ya hapo awali

23:43 - May 07, 2023
Habari ID: 3476970
TEHRAN (IQNA) – Jamii ya wanadamu leo ina kiu ya mafundisho ya Mwenyezi Mungu ya Qur’ani Tukufu zaidi kuliko hapo awali, mwanazuoni mwandamizi wa Kiislamu nchini Iran amebaini.

Katika ujumbe kwa Tamasha la Qur’ani na Etrat la Chuo Kikuu cha Payam Noor, Ayatullah Jafar Sobhani alisisitiza kwamba Qur'ani Tukufu bila shaka ni hazina ya ukweli kwa ulimwengu huu na ujao na nichemchemi ya maisha ya Mwenyezi Mungu.

Alisema pamoja na kuwa kufika katika kina cha mafundisho ya Qur’ani si jambo rahisi, kila mtu anaweza kufaidika na fikra na mafundisho yake ili kujiinua yeye na jamii.

Ayatullah Sobhani amewataka vijana kudumisha na kuimarisha mafungamano yao ya kiroho na Kitabu hicho Kitukufu na kuweka  utekelezaji wa mafundisho yake katika ajenda zao.

Aidha amepongeza kuandaliwa kwa tamasha la Qur'ani na Etrat la Chuo Kikuu cha Payam Noor na kuwasifu wanafunzi walioshiriki katika hafla hiyo ya Qur'ani.

Toleo la 26 la tamasha hilo lilifanyika kaskazini-magharibi mwa jiji la Tabriz mapema wiki hii.

Chuo Kikuu cha Payam Noor kutoka miji mbalimbali ya nchi kilishiriki katika tamasha hilo, kikishindana katika kategoria 40 kama vile kuhifadhi Qur'ani, usomaji, Nahj al-Balagha, Sahifeh Sajjadiyeh, uvumbuzi wa Qur'ani, sanaa na fasihi.

4138975

Kishikizo: qurani tukufu sobhani
captcha