IQNA

Uislamu na Ukristo

Mkuu wa seminari za Kiislamu Iran akutana na Papa Francis

15:32 - May 31, 2022
Habari ID: 3475317
TEHRAN (IQNA) – Mkurugenzi wa Vyuo vya Kiislamu Iran Ayatullah Alireza Arafi alikutana na kufanya mazungumzo na Papa Francis.

Mkutano huo ulifanyika Jumanne asubuhi katika makao mkauu wa Kanisa Katoliki Duniani huko Vatican.

Viongozi hao wawili wa kidini waliashiria umuhimu wa kuimarisha uhusiano kati ya dini na kulaani dhuluma dhidi ya watu kote ulimwenguni.

Ayatullah Arafi anatembelea Vatican na Italia kwa mwaliko rasmi wa vituo vya kielimu vya nchi hiyo.

Mapema katika barua mbili tofauti, maulama mashuhuri wa Kishia Ayatullah Makarem Shirazi na Ayatullah Jafar Sobhani walikuwa wamekaribisha safari hiyo, wakimtaka Ayatullah Arafi kutafuta njia za kupanua ushirikiano na Vatican katika nyanja mbalimbali zenye maslahi kwa pande zote. 

captcha