IQNA

Sura za Qur’ani Tukufu /77

Onyo Kali kwa Wakanushaji wa Siku ya Kiyama katika Surah Al-Mursalat

13:20 - May 16, 2023
Habari ID: 3477006
TEHRAN (IQNA) – Mwenyezi Mungu katika aya nyingi za Qur’ani Tukufu amesisitiza juu ya kuja kwa Siku ya Kiyama na akawaonya wale wanaoikadhibisha.

Hata hivyo, katika Sura moja ya Kitabu kitukufu onyo hili limerudiwa mara kumi, jambo ambalo linaonyesha ukali wa onyo hilo. Na hiyo ndiyo Surah Al-Mursalat.

Al-Mursalat ni jina la sura ya 77 ya Qur’ani Tukufu, ambayo ina aya 50 na iko katika Juzuu ya 29

Ni Makki na Sura ya 33 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad(SAW).

Mwanzoni mwa Sura, Mwenyezi Mungu anaapa kwa Mursalat (mitume, wale waliotumwa), na kwa hivyo jina la sura. Mursalat inasemekana kuwa ni malaika walioleta ufunuo au dhoruba zilizotumwa.

Katika Sura hii, Mwenyezi Mungu anaapa kwa mambo matano muhimu sana: “ Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole!  Na zinazo vuma kwa kasi! Na zikaeneza maeneo yote!  Na zinazo farikisha zikatawanya! Na zinazo peleka mawaidha!  (Aya za 1-5)

Sura inasisitiza sana kutokea kwa Siku ya Kiyama na dalili zake na pia inazungumzia neema za Mwenyezi Mungu walizopewa wanadamu pamoja na matendo na dalili za wafanyao wema na waovu na hatima yao.

Katika sura hii, msisitizo wa Siku ya Kiyama unakuja na onyo kali kwa wale wanaoikadhibisha.

Maneno "Siku hiyo, ole wao waliozikataa Aya za Mwenyezi Mungu!" imerudiwa mara kumi katika Sura hii, ili kwamba hakuna yeyote atakayekuwa na uhalali wowote wa kuikataa Siku ya Hukumu.

Kulingana na Allamah Tabatabai, mwandishi wa Tafsiri ya Qur’ani ya Al Mizan, Siku ya Kiyama inajumuisha matukio ambayo yangemaanisha mwisho wa ulimwengu wa mwanadamu. Kwa maoni yake, aya ya 8 hadi 12 za Sura zinazotaja baadhi ya matukio ya siku hiyo kama vile nyota kupoteza nuru yake, mbingu kupasuliwa, na kupeperushwa milima kuwa vumbi, ni dalili kwamba maisha ya mwanadamu yataisha siku hiyo.

captcha