IQNA

Ukombozi wa Palestina

Harakati ya Hamas ya Palestina yashukuru Iran, Hizbullah kwa msaada

13:25 - May 16, 2023
Habari ID: 3477007
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema: "Tunazishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Hizbullah ya Lebanon kwa namna ya kipekee."

Televisheni ya al Mayadeen imemnukuu Ismail Hania akisema hayo jana baada ya utawala wa Kizayuni wa Israel kulazimika kukubali usimamishaji vita vya siku tano ulivyovianzisha Jumanne ya wiki iliyopita dhidi ya wananchi wa Ghaza.

Katika sehemu moja ya matamshi yake, Ismail Hania amesema, anayapongeza makundi ya muqawama ya Palestina kwa kusimama imara kukabiliana vilivyo na uvamizi wa hivi karibuni wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Ghaza, kama ambavyo anawashukuru wale wote waliokuwa pamoja na taifa la Palestina muda wote huo na hasa hasa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Hizbullah ya Lebanon.

Jumanne ya wiki iliyopita, jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Isael lilianzisha mashambulio dhidi ya Ukanda wa Ghaza na kuendelea kushambulia maeneo mbalimbali ya ukanda huo hadi Ijumaa. Lakini makundi ya muqawama ya Palestina yalisimama kidete kukabiliana na jinai hizo. Yaliendesha operesheni ya kishujaa iliyopewa jina la "Kisasi cha Watu Huru" na kupiga kwa makombora maeneo ya ndani kabisa ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni yakiwemo maeneo ya Baytul Muqaddas Magharibi.

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS pia amesema, makundi ya muqawama ya Palestina yalidhibiti hali ya mambo kwa ushirikiano wao imara, na kutoa majibu makali kwa walowezi wa Kizayuni katika kipindi chote cha siku tano za vita hivyo vipya vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni.

4140947

captcha