IQNA

Tafsiri ya Qur'ani

Mwanazuoni wa Pakistani akamilisha Tafsiri ya Kiingereza ya Qur'anI Tukufu

16:56 - May 19, 2023
Habari ID: 3477017
TEHRAN (IQNA) – Tahirul Qadri, mwanazuoni mashuhuri wa Pakistani, amekamilisha tafsiri ya Kiingereza ya Quran Tukufu.

Tafsiri hiyo itachapishwa katika mwezi huu, msemaji wa Taasisi ya Tehreek Minhajul Qur'an (TMQ) - ambayo imeanzishwa na Qadri - alisema, The News International iliripoti.

Sherehe za kuzinduliwa kwa Tarjuma ya Qur'ani kwa Kiingereza kwa jina la ‘Dhihirisho la Qur’ani’ zitafanyika katika Kambi ya al-Hidayah ya Uingereza mwezi wa Agosti na kuzinduliwa kwake nchini Pakistani kutafanyika baadaye, msemaji huyo alisema.

Qadri anashikilia sifa ya kuwa mtu wa kwanza katika ulimwengu wa Kiislamu kutafsiri Qur'ani Tukufu katika lugha mbili. Hapo awali alitafsiri Qur'ani Tukufu kwa Kiurdu na sasa Dk Qadri ameitafsiri Qur'ani moja kwa moja kutoka Kiarabu hadi Kiingereza cha kisasa.

Tafsiri hii ni ya kipekee kwani inatumia lugha ya Kiingereza iliyo rahisi kueleweka ambayo inafundishwa, kusomwa na kuzungumzwa na wanafunzi na makundi mengine ya jamii.

Mwanasiasa wa zamani na mwanzilishi wa Minhaj-ul-Quran na Pakistan Awami Tehreek, Muhammad Tahir-ul-Qadri alizaliwa Februari 19, 1951. Ni mwanazuoni wa Kiislamu kutoka Pakistan ambaye ana pia uraia wa Kanada. Pia amewahu kufundisha sheria ya kimataifa ya katiba katika Chuo Kikuu cha Punjab. Alianzisha asasi ndogondogo mbalimbali chini ya Minhaj-ul-Quran International. Amekuwa akishirikishwa katika Orodha ya Waislamu Mashuhuri Duniani ya The 500 Most Influential Muslims kila mwaka tangu kuanzishwa kwake 2009.

3483614

captcha