IQNA

Tarjuma ya Qur'ani

Tarjuma mpya ya Qur’ani kwa lugha ya Kifaransa

10:56 - June 13, 2022
Habari ID: 3475370
TEHRAN (IQNA)- Tarjuma mpya ya Qur’ani Tukufu kwa lugya ya Kifaransa imechapishwa nchini Algeria.

Waalgeria wawili, mmoja ambaye ni mtaalamu wa tarjuma pia ni mwandishi habari na mwingine ambaye ni mtafiti nwa mwanazuoni wa Kiislamu wameshirikiana katika kutayarisha tarjuma mpya ya Qur’ani Tukufu kwa lugha ya Kifaransa.

Wanasema lengo lao ni kujaza mapengo yaliyo katika tarjumai zilizotangulia za Kifaransa  na pia wameongeza maelezo mafupi kuhusu maana ya aya.

Taarjuma hiyo ya Qur’ani iliotayarishwa na Mtafiti na mwanazuoni wa kidni Sheikh Kamal Shakat pamoja na mwandishi habari Masoud Bu Junun imechapishwa na Shirika la Uchapishaji la al Bayazeen.

Katika tarjuma hii wameashiria tarjuma zilizotangulia za Qur’ani ikiwemo ya Kilatini iliyotayarishwa mwaka 1141 Miladia na ile ya kale zaidi ya Kifaransa iliyoandikwa mwaka 1647 Miladia.

Wawili hao wamefanya utafiti kuhusu kazi za watafiti na wasomi wengine wa Algeria kama vile Sheikh Hamza Bubakr na Ahmed al-Amish.

Tarjuma mpya itawanufaisha wanaozungumza Kifaransa, wewe ni Waislamu au wasiokuwa Waislamu, ili wawezi kufahamu aya za Qur’ani kwa ubora zaidi.

Bu Junun ametarjumu vitabu 20 kwa lugha ya Kifaransa katika nyuga za fikra na sayansi za Kiislamu. Sheikh Shakati ni mtaalamu wa masuala ya Kiislamu na anazungumza Kifaransa, Kitaliano, na Kijerumani na hutoa mihadhara katika televisheni na redio za Ufaransa.

4063694

captcha