IQNA

Chuki dhidi ya Waislamu

Waislamu nchini Ufini wataka zichukuliwe dhidi ya ubaguzi wa rangi, matamshi ya chuki

16:39 - July 18, 2023
Habari ID: 3477300
HELSINKI (IQNA) – Mashirika ya Kiislamu Ufini (Finland) yameihimizwa serikali ya nchi hiyo kuchukua hatua kali za "kutovumilia" ubaguzi wa rangi.

"Tunatoa wito kwa serikali ya Ufini na hasa Waziri Mkuu Petteri Orpo (NCP) kuwa na bidii zaidi katika kukemea uhalalishaji wa matamshi ya wazi ya chuki na kuchukua hatua ya kutokomeza mawazo ya kibaguzi," walisema katika taarifa ya pamoja.

Kumekuwa na mjadala katika vyombo vya habari vya Ufini tangu wiki iliyopita baada ya Rais Sauli Niinistö kusema kuwa "ingekuwa busara kuchukua msimamo wa kutovumilia ubaguzi wa rangi" ili kujibu maoni ya ubaguzi wa rangi na vurugu yaliyoandikwa na Waziri wa Fedha na Naibu Waziri Mkuu Riikka Purra (Finns) kwenye blogu mnamo 2008.

Taarifa hiyo pia ilirejelea maoni ambayo Purra aliandika kwenye blogi yake mwenyewe mnamo 2019 akikosoa jinsi wanawake wa Kiislamu wanavaa, ambayo mashirika ya Kiislamu yalielezea kama ubaguzi wa rangi, udhalilishaji na ubaguzi kwa sauti.

Purra ameomba msamaha kwa maoni aliyoandika mnamo 2008, lakini hajatoa msamaha kwa maandishi ya 2019 kwenye blogi yake mwenyewe.

Waziri Mkuu Orpo alisema amejadili chapisho la blogi la 2019 na Purra, na kuongeza kuwa yeye mwenyewe hatatumia lugha ile ile ambayo Purra alitumia kwenye maandishi.

Taarifa hiyo - ambayo imetiwa saini na jumla ya jumuiya na mashirika 26 ya Kiislamu - pia ilitaja sheria ya Ufini kuhusu uhuru wa dini ambayo inabaini kuwa kila mtu ana haki ya kufuata dini yake mwenyewe.

"Hii ni pamoja na uhuru wa kuvaa kulingana na dini ya mtu," taarifa hiyo ilibainisha.

3484382

Kishikizo: finland ufini waislamu
captcha