IQNA

Balozi wa Ufini aelezea Tajiriba yake ya kuvaa Hijabu katika Haram ya Imam Hussein (AS)

21:04 - April 29, 2025
Habari ID: 3480609
IQNA – Auno Saarela, balozi wa Ufini (Finland) nchini Iraq, hivi karibuni alitembelea Haram ya Imam Hussein (AS) huko Karbala, ambapo alishiriki tajiriba yake ya kuvaa hijabu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Noon la Iraq, Saarela alitembelea eneo hilo takatifu na kupewa maelezo kuhusu miradi mbalimbali inayoendeshwa na uongozi wa haram hiyo. Aliisifu huduma nyingi zinazotolewa kwa mahujaji wakati wa ziara yake.  

Akizungumza kuhusu maoni yake, Saarela alielezea tajiriba hiyo kama nzuri sana. "Ziara ilikuwa nzuri kweli, na Haram ya Imam Hussein ni mahali pa kuvutia sana," alisema.  

Akirejelea vipengele vya kitamaduni vya ziara yake, Saarela aligusia tajiriba yake ya kuvaa mavazi ya kitamaduni. "Mwenzangu alinisaidia katika hili," alisema kuhusu kuvaa hijabu na abaya. "Nilikuwa nimetembelea Najaf hapo awali, kwa hiyo nilikuwa tayari nimezoea kuvaa abaya."  

Saarela amekuwa akihudumu kama balozi wa Ufini nchini Iraq tangu 2023.  

Haram ya Imam Hussein (AS), moja ya maeneo muhimu ya ibada kwa Waislamu wa madhehebu ya Shia, huvutia mamilioni ya wageni kila mwaka, hasa wakati wa kumbukumbu kubwa za kidini kama Arbaeen.

3492871

captcha