IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

ISESCO yazindua kampeni ya kukabiliana na kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu

20:15 - August 26, 2023
Habari ID: 3477498
RABAT (IQNA) - Shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi na Utamaduni Duniani (ISESCO) lilianzisha kampeni yenye lengo la kukabiliana na dhulma za Qur'ani katika nchi za Magharibi.

Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, Salim bin Mohammed Al Malik, alizindua mpango huo, uliopewa jina la "Isome ili Uielewe", katika hafla ya ufunguzi wa mkutano wa kimataifa huko Rabat, Morocco.

Amesema, kwa mapana, usahihi na uzito wake, kampeni hiyo ni jibu chanya kwa vitendo vya uvunjifu wa heshima dhidi ya matukufu ya Kiislamu.

Wanazuoni na maprofesa wa vyuo vikuu kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu walishiriki katika mkutano huo wa kujadili uhuru unaozingatia maadili ya Kiislamu na sheria za kimataifa.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa la Waislamu (MLW) Muhammad bin Abdul Karim Issa alikuwa mmoja wa wazungumzaji katika hafla hiyo.

Alisisitiza kuwa uhuru hauwezi kuwa bila sheria na mipaka. Pia alisisitiza kwamba Uislamu unadhamini uhuru na haki.

Katika wiki za hivi karibuni, kuchafuliwa kwa Qur'ani katika nchi kadhaa za Ulaya, zikiwemo Uswidi na Denmark, kwa idhini ya serikali na ulinzi wa polisi kumezusha hasira na shutuma nyingi kutoka kwa ulimwengu wa Kiislamu.

Nchi hizo za ukandwa wa Skandinavia zinaruhusu kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu chini ya kivuli cha kile kinachoitwa kuwa eti ni uhuru wa kujieleza licha ya kulaaniwa na mataifa ya Kiislamu na yasiyo ya Kiislamu na hata mbele ya azimio la Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa dhidi ya vitendo vya kufuru.

3484922

Kishikizo: isesco qurani tukufu
captcha