IQNA

Zifahamu Dhambi/5

Njia ya Kujua Dhambi

21:20 - November 04, 2023
Habari ID: 3477841
TEHRAN (IQNA) – Katika Qur'ani Tukufu, makundi 18 ya watu yamelaaniwa kwa kufanya madhambi tofauti.

Kwa kusoma visa vya watu hawa, tunaweza kutambua aina tofauti za dhambi.

La’an (kulaani) maana yake ni kusukuma mbali na rehema. Imechanganyika na hasira na ghadhabu.

Ukweli ni kwamba rehema ya Mungu ni pana na inajumuisha yote: “...Rehema Yangu inakumbatia vitu vyote...” (Aya ya 156 ya Surat Al-A’araf)

Hata hivyo, baadhi ya watu wanafanya chaguo lisilofaa na kupotea, na kufikia hatua ya kuwa kama mpira kwenye bahari ya rehema ya kimungu ambao hakuna maji yanayoweza kuingia.

Waliolaaniwa ndani ya Qur'ani Tukufu ni pamoja na makafiri, washirikina, Mayahudi makaidi, walioritadi, wavunja sheria wadanganyifu, wanaovunja ahadi, wanaoficha ukweli, wanafiki, waliomuudhi Mtukufu Mtume (SAW), madhalimu, wauaji, Iblis (Shetani), wale wanaowatuhumu wanawake waliotakasika, wapinzani wa viongozi wa kweli wa jamii ya Kiislamu, waongo, na wanaoeneza uvumi na taarifa bandia.

 

Katika Hadithi za Kiislamu pia, baadhi ya watu wamelaaniwa, ikiwa ni pamoja na:

Wale waliopotosha vitabu vya kimungu.

Wale ambao hawakubali aliyo yaamuru Mwenyezi Mungu.

Wale wanaotukana Nyumba ya Mtukufu Mtume (SAW) yaani Ahul Bayt.

Ambao wanaopora yaliyo ya wapiganaji katika Njia ya Mwenyezi Mungu.

Wale wanaowaambia watu watende mema lakini wao wenyewe hawafanyi mema, au wanaowaambia wengine wasifanye mabaya huku wao wenyewe wakiyafanya.

Kishikizo: dhambi
captcha