IQNA

Zifahamu Dhambi/1

Kwa Nini Ni Muhimu Kujua Dhambi?

15:42 - October 25, 2023
Habari ID: 3477785
TEHRAN (IQNA) – Mtu anatakiwa kuzingatia mambo ambayo yanamdhuru kiakili, kiroho na kimwili, ili kujiepusha nayo na kukaa bila kudhurika.

Hebu wazia bustani mbili za jirani ambazo ziko katika hali sawa ya hewa, zina mimea sawa, na hupokea kiasi sawa cha maji na mwanga. Mtunza bustani wa kwanza ni mwangalifu sana na haruhusu magugu kukua na hivyo mimiea yake haipati madhara. Mimea katika bustani hii kwa hakika iko katika hali nzuri, na imejaa maua na matunda.
Bustani nyingine, kwa upande mwingine, ina mtunza bustani ambaye hajali au hajui nini kinachodhuru mimea. Matokeo yake ni bustani iliyonyauka isiyo na maua huku matunda yake yakiwa yameharibiwa na wadudu.
Binadamu wako hivyo pia. Wasipozingatia yale yanayowadhuru kiakili, kiroho na kimwili, watageuka na kuwa watu wa kutisha, lakini ikiwa watakuwa waangalifu wasiruhusu mambo hayo yawadhuru, watakuwa watu wenye heshima na ufanisi.
Kinachowadhuru wanadamu kiroho ni dhambi na maovu ya kimaadili na mitume wote wa Mwenyezi Mungu na vitabu vya Mwenyezi Mungu vimetuusia kuziepuka. Imam Ali (AS) alisema: Kinachodhuru nafsi na roho ya mwanadamu ni ubakhili na kushikamana na dunia.
Na imepokewa kutoka kwa Imamu Sadiq (AS) kwamba kinachodhuru dini na imani ni husuda, ubinafsi na majivuno.

Kishikizo: dhambi
captcha