IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Waafrika washinda mashindano ya Kimataifa la Qur'ani kwa wanawake la Dubai

17:46 - October 09, 2022
Habari ID: 3475905
TEHRAN (IQNA) – Hafla ya kufunga toleo la 6 la tuzo ya Kimataifa ya Qur’ani ya Sheikha Fatima Bint Mubarak kwa wanawake ilifanyika Dubai ambapo washindi walipokea tuzo zao.

Wametangazwa katika hafla ya kufunga mashindano hayo iliyofanyika Jumamosi usikumjini Dubai na kuwaleta pamoja washiriki pamoja na maafisa wa Umoja wa Falme za Kiarabu na waandaaji wa shindano hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa mashindano hayo  ya kuhifadhi Qur'ani Aminat al Dabus amesema watu 50 kutoka nchi 50 walishiriki katika mashindano hayo yenye lengo la kuwahimiza vijana kuhifadhi Qur'ani Tukufu.

Aindati Sisi kutoka Senegal alinyakua nafasi ya kwanza huku Ayeshah Abubakr Hasan kutoka Nigeria na Shima Anfal Tabani kutoka Algeria akifuata.

Mashindano hayo yalihitimishwa Jumatano jioni katika Jumuiya ya Utamaduni na Sayansi ya Dubai.

Kwa mujibu wa waandaaji, washindani hao walikuwa na umri wa chini ya miaka 25 na wahifadhi Qur'ani nzima kwa umahiri wa sheria za Tajweed.

Mshindi bora wa shindano hilo alipata pesa taslimu dirham 250,000 huku walioshika nafasi ya pili hadi kumi wakipewa dirham 200,000 hadi 35,000.

Tuzo ya Kimataifa ya Dubai ya Qur'ani Tukufu (DIHQA) kila mwaka huandaa hafla ya kimataifa ya Qur'ani kwa wanawake kutoka nchi mbalimbali.

4090281

Habari zinazohusiana
Kishikizo: dihqa qurani tukufu
captcha