IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu /22

Sura Al-Hajj; Onyo dhidi ya Mabishano juu ya Mungu

14:26 - October 20, 2022
Habari ID: 3475960
TEHRAN (IQNA) – Katika aya mbalimbali za Qur'ani Tukufu, Mwenyezi Mungu amewapa changamoto wale wanaokataa ujumbe wa Wake, wale ambao walikuwa makafiri au washirikina. Mwenyezi Mungu anawapa changamoto ya kuunda chembe au kuleta aya inayofanana na ile ya Qur'ani Tukufu lakini hakuna aliyeweza kufanya hivyo.

Ndio maana Surah Al-Hajj inawaonya watu kuwa na khofu ya Mwenyezi Mungu na waepuke kubishana juu ya Mwenyezi Mungu na wamfuate kila shetani muasi.

Surah Al-Hajj ni sura ya 22 ya Qur'ani Tukufu ambayo ina aya 78 na iko katika Juzuu ya 17. Ni Sura ya 103 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Neno Hajj maana yake ni nia ya kufanya jambo fulani na katika Uislamu linarejelea Ibada ya Hija ya kila mwaka huko Makka. Kwa kuwa aya 13 za Sura (25 hadi 37) zinahusu Kaaba, historia yake na athari za kijamii na kisiasa za Hija, jina la sura hii ni Al-Hajj.

Sura imeanza kwa Aya inayowakumbusha watu Siku ya Kiyama na tetemeko lake la ardhi: “ Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi. Hakika tetemeko la Saa (ya Kiyama) ni jambo kuu.”

Maudhui ya jumla ya Sura ni kuhusu sifa na hatima ya waumini na makundi kadhaa ya makafiri. Kundi la kwanza la makafiri ni wale ambao, bila ya kuwa na ujuzi wowote, wanazungumza kuhusu sifa za Mwenyezi Mungu na anayoyafanya na wanawatii mashetani. Hatimaye, mashetani hao watapelekea wakumbwe na hatima ya adhabu na moto.

Kundi la pili ni wale wanaotaka kuwapoteza wengine. Hao ambao ni viongozi wa Mushrikeen (washirikina) wataishia kupata adhabu ya kufedhehesha Siku ya Kiyama. Kundi la tatu ni wale wanaojifanya kuwa wanamwabudu Mungu lakini imani yao inabadilikabadilika kadiri wanavyopata amani kila wanaposikia habari njema lakini wanajitenga na Mungu wakati wowote kunapokuwa na dhiki au shida. Kundi hili nalo ni miongoni mwa waliopata hasara.

Kwa upande mwingine, kuna waaminifu ambao wamepewa cheo cha juu na Mwenyezi Mungu.

Pia, baadhi ya aya za Sura hii zinazungumzia Tauhidi na haja ya kumwabudu Mwenyezi Mungu Mmoja, kuonya dhidi ya ushirikina na matokeo yake, na kubainisha uhakika wa Siku ya Kiyama na tetemeko lake la kutisha.

Sura hiyo pia ina aya zinazohusu vipengele tofauti vya kiroho na Fiqhi vya Hija, Jihad dhidi ya madhalimu, kusali sala, kutoa Zaka na kukuza wema na kuzuia maovu.

Pia inafafanua baadhi ya maadili ya kimaadili kama vile Tawakkul (kuweka imani kwa Mungu), inaonya dhidi ya kutenda dhambi na kutomtii Mwenyezi Mungu, na inasisitiza uhusiano kati ya Taqwa (kumcha Mungu), matendo mema na msaada wa kimaanawi.

Habari zinazohusiana
captcha