IQNA

Ufundishaji Qur'ani Tukufu

Mtoto wa miaka 4 akimfundisha Qur'ani dada yake mwenye umri wa miaka 3 (+Video)

21:08 - October 14, 2022
Habari ID: 3475928
TEHRAN (IQNA) – Klipi ya video inayomuonyesha mtoto wa miaka minne akimfundisha Qur'ani ndugu yake wa miaka mitatu imesambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Katika klipu hiyo, msichana mdogo anasoma aya ya Surah Ash-Shams ya Qur'ani Tukufu huku kaka yake akirekebisha usomaji wake.

Klipu hiyo imetumwa imesambazwa na watumizi wengi wa mitandao ya kijamii huku maelefu wakibonyesha ishara ya kuipenda.

Watumiaji wa Twitter wamepongeza juhudi za familia hiyo za kuwafunza watoto wao wachanga Qur'ani katika umri mdogo.

Wamebainisha kuwa, Kitabu kitukufu ni nuru inayowaongoza kwenye njia sahihi ya maisha na kwamba kuwafunza watoto Qur’ani ni jambo jema linalostahiki malipo ya Mwenyezi Mungu.

Wataalamu na walimu wanaamini kuwa wakati mzuri wa kujifunza Qur'ani Tukufu ni katika umri mdogo.

Pia wanasema watoto huwafuata wazazi wao kama kielelezo cha kuigwa katika kujifunza na kutenda kulingana na mafundisho ya Qur'ani Tukufu.

4091399

Kishikizo: watoto qurani tukufu
captcha