IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

San Francisco: CAIR yaalaani chuki dhidi ya Uislamu wakati wa Eid Al-Adha

10:56 - June 20, 2024
Habari ID: 3478992
IQNA-Baraza la Uhusiano wa Uislamu na Marekani (CAIR) eneo la San Francisco Bay Area (CAIR-SFBA) limelaani vikali mashambulizi ya maneno ya chuki yaliyolenga jamii ya Waislamu wakati wa Eid Al-Adha.

 Tukio hilo lilitokea wakati Waislamu wakiwa katika Kituo cha Kiislamu cha San Francisco walipokusanyika kwa ajili ya sala ya Eid al-Adha katika McLaren Park siku ya Jumatatu.

 Video ya tukio inaonyesha mtu mmoja akitoa maneneo ya kibaguzi na chuki dhidi ya Uislamu kuelekea kundi hilo, Mwanaume huyo amerekodiwa akisema, “Dini yenu imejaa chuki,” na akaendelea na kauli za dharau zaidi, zikiwemo za matusi na kuwaita waliohudhuria “mashetani”.

 Zahra Billoo, Mkurugenzi Mtendaji wa CAIR-SFBA, alijibu tukio hilo, akisema, "Aina hii ya matamshi ya chuki haikubaliki na inapaswa kulaaniwa kwa maneno makali," tovuti rasmi ya kundi hilo iliripoti siku ya Jumanne.

 “Jumuiya ya Waislamu, kama jumuiya nyingine yoyote, ina haki ya kukusanyika na kuabudu kwa amani, Matukio kama haya yanasaidia tu kusisitiza haja ya dharura ya kukabiliana na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu katika taifa letu.

Billoo pia alisisitiza athari pana zaidi za kijamii za uhasama huo, akitoa wito wa umoja na hatua dhidi ya chuki, "uadui na ujinga wa aina hii sio tu una madhara kwa walengwa moja kwa moja bali hata kwa jamii kwa ujumla kwani unaleta mifarakano na kutovumiliana.

Na pia tunawaomba viongozi wa jumuiya, viongozi wa umma na watu wote wenye dhamiri kusimama pamoja nasi kukemea vitendo hivyo vya chuki dhidi ya Uislamu.

 'Islamophobia (chuki dhidi ya Uislamu) ni Kweli na Inaumiza

Shahbaz Shaikh, Mjumbe wa Bodi ya Kituo cha Kiislamu cha San Francisco, alielezea mshtuko wake na wasiwasi wake juu ya tukio hilo, akielezea juu ya hali yake isiyo ya kawaida katika jamii na maonyesho ya kawaida ya ubaguzi wa rangi na chuki ya wageni.

 Tukio hilo linalingana na ripoti ya hivi majuzi ya CAIR, ambayo ilirekodi idadi kubwa zaidi ya matukio ya chuki dhidi ya Uislamu katika historia ya shirika hilo.

 Ripoti hiyo inataka hatua za haraka zichukuliwe kukabiliana na hisia zinazoongezeka dhidi ya Uislamu, ambazo zimekua hasa baada ya kuanza kwa vita vya utawala katili wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza mwezi  Oktoba tarehe 7, mwaka jana.

 

3488810

captcha