IQNA

Sikukuu ya Eid Ghadir Khum

Matukio ya sherehe za Sikukuu ya Eid Ghadir yaliyojengwa kwa Njia ya Kuendeleza Utawala wa Kiislamu

8:33 - June 26, 2024
Habari ID: 3479012
Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo amekutana na kuzungumza na maelfu ya wananchi katika sherehe ya maadhimisho ya Sikukuu ya Eid Ghadir Khum.

Leo Jumanne tarehe 18 Dhulhija mwaka 1445 Hijria ambayo ni sawa na Juni 25 mwaka 2024 Miladia ni Sikukuu ya Eid Ghadir Khum ambayo ni Idd kubwa ya Waislamu duniani. 

Tovuti ya habari ya ofisi ya kuchapisha na kuhifadhi kazi za Ayatollah Khamenei imeripoti kuwa, Kiongozi Muadhamu leo asubuhi amekutana na kuzungumza na maelfu ya watu kutoka mikoa ya Gilan, wa Kati, Kohkiluyeh na Boyer-Ahmad na Khorasan Kaskazini pamoja na familia za mashahidi na wahudumu wa Haram Tukufu la Hadhrat Ahmad bin Musa (AS) maarufu kama Shah Cheragh kutoka mkoa wa Farsi katika maadhimisho ya Sikukuu ya Eid Ghadir-Khum na katika kukaribia uchaguzi wa 14 wa Rais wa Iran.

Hafla hiyo ya Sikukuu ya Eid Ghadir Khum imefanyika katika Husseiniya ya Imam Khomeini (MA). 

captcha