Imam Husein (AS) alipoombwa kukubali Baiyat (utiifu) ya Yazid bin Muawiyyah, sio tu hakuikubali, bali pia alianzisha mageuzi yenye nuru ili kuuokoa Umma wa Mtume (SAW) kutokana na uzushi na upotofu uliyosababishwa na utawala wa Yazid.
Je, mauaji hayo yalikubalika kwa mtazamo wa Qur’ani Tukufu? Kwa maneno mengine, ni aya zipi za Qur’ani zinazoidhinisha harakati hii na ni misingi gani ya Qur'ani inayoweza kuielezea?
Ushahidi bora zaidi wa msingi wa Qur'ani wa uasi wa Imam Hussein (AS) unaweza kupatikana katika wasia wake ulioandikwa kwa ndugu yake Muhammad ibn al-Hanafiyya.
Imam (AS) aliandika katika wasia huo: “Sikuinuka kwa kiburi au kwa kutaka badala ya kuurekebisha Umma wa babu yangu Muhammad. Nataka kuamrisha mema na kukataza maovu na kutenda kwa mujibu wa Siira na Sunnah za babu yangu na njia ya baba yangu Ali ibn Abi Talib (AS).”
Katika wosia huu, yametajwa masuala kadhaa ambayo yanaonesha Imam Hussein (AS) aliinuka dhidi ya dhulma kwa kuzingatia mafundisho ya Qur'ani. Lengo la kwanza la Imam Hussein (AS) lilikuwa ni kuurekebisha Umma wa Mtume (SAW).
Kwa hakika, moja ya majukumu ya msingi na misheni ya manabii wa Mwenyezi Mungu ni kurekebisha jamii. Mitume wa Mwenyezi Mungu, kwa rehema na huruma, waliwaonya watu wao dhidi ya ufisadi na kujaribu kuwafikisha kwenye njia iliyonyooka ili jamii isiharibike na ufisadi wa baadhi ya watu.
Nabii Shuaib (AS), kwa mfano, alisema lengo lake lilikuwa mageuzi kadiri iwezekanavyo: “Natafuta lakini kurekebisha kadiri niwezavyo, msaada wangu unatoka kwa Mwenyezi Mungu pekee. Kwake nimemtegemea na kwake Yeye narejea katika toba , Aya ya 88 ya Surah Hud.
Harakati ya Imam Hussein (AS) Katika Qur’ani Tukufu
Hata hivyo, ni wazi kuwa kuirekebisha jamii haiwezekani isipokuwa watawala wa jamii warekebishwe.
Mwenyezi Mungu alipomteua Musa (AS) kuwa utume, hakumtuma kwa watu wa Misri tu bali pia kwa Firauni, na akamwambia Musa (AS): “Nenda kwa Firauni, amejivuna.” (Aya ya 24 ya Surah Taha)
Kiburi na kuvuka mipaka kwa watawala ndio sababu kuu ya ufisadi wa jamii, na warekebishaji wa jamii wanajaribu kutatua tatizo hili kwanza.
Makabiliano ya Imam Hussein (AS) na Yazid ibn Muawiyyah yalikuwa ya aina hii.