IQNA

Harakati za Qur'ani

Iran yazindua mpango wa kuimarisha kuhifadhi Qur'ani miongoni mwa wanafunzi

21:46 - November 26, 2024
Habari ID: 3479814
IQNA - Maafisa wa Iran wamezindua mipango miwili mipya yenye lengo la kuhimiza kuhifadhi wa Qur'ani Tukufu miongoni mwa wanafunzi kote nchini.

 

Uzinduzi wa suhula mbili muhimu za elimu ya Qur’ani—Kitabu cha Mbinu za Kuhifadhi Qur’ani na aplikesheni ay appu ya "i-League"—ulifanyika Jumatatu, Novemba 25, mjini Tehran.

Mpango huo ni juhudi za pamoja kati ya Wizara ya Elimu ya Iran na Jumuiya ya Maendeleo ya Kiislamu, kwa lengo la kuimarisha kuhifadhi Qur’ani na kuielewana miongoni mwa wanafunzi wa shule nchini kote.

Katika hafla hiyo, Waziri wa Elimu Alireza Kazemi alisifu ushirikiano kati ya mashirika hayo mawili katika kukuza utamaduni wa Qur'ani miongoni mwa wanafunzi. "Kuifahamu Quran na kuhifadhi aya zake kunapaswa kuhusisha kutumia rasilimali zote zilizopo," Kazemi alisema.

Mpango huo unajumuisha usambazaji wa vitabu 200,000 vyenye Juzuu Amma ya Qur’ani Tukufu. Vitabu hivi vya kazi vitawekwa madarasani, huku walimu wakiwasaidia wanafunzi kuhifadhi katika mwaka mzima wa masomo.

Wanafunzi waliofaulu wataingia kwenye vituo vya juu vya Qur'ani kwa masomo zaidi.

Apu ya "i-League", iliyoundwa kwa ajili ya Android, ina jukwaa shirikishi la mashindano ya Qur’ani katika viwango vya mikoa na kitaifa. Wanafunzi wanaweza kushiriki katika changamoto za kikundi huku walimu wakifuatilia maendeleo ya mtu binafsi. "Suhula hii inahakikisha mwingiliano wa maana na maudhui ya Qur'ani huku ikikuza ushindani mzuri miongoni mwa wanafunzi," alieleza Hujjatul-Islam Majed Manabi, mkuu wa Idara ya Qur’ani, Etrat na Swala katika Wizara ya Elimu ya Iran.

Hujjatul Islam Mohammad Qomi, Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kiislamu, alisisitiza dhamira pana ya mpango huo: “Watu wengi wanaiheshimu sana Qur’ani Tukufu, lakini mafundisho yake mara nyingi yanawekwa kando. Lengo letu ni kuunganisha elimu ya Qur'ani katika maisha ya wanafunzi kwa njia zinazoweza kufikiwa."

Mpango huu unawiana na juhudi pana zaidi za kufikia dira ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya kutoa mafunzo ya kuwezesha kuwepo watu milioni 10 waliohifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu nchini Iran.

4250377

Habari zinazohusiana
captcha