"Mamlaka ya utawala katili wa Israel yanatafuta mara kwa mara kubadilisha sura za msikiti na Wayahudi," alisema Ghassan Al-Rajabi, afisa wa mamlaka ya wakfu wa jiji hilo, katika mahojiano na Anadolu.
Alitaja kitendo hicho kama "shambulio kubwa" kwenye sehemu ya ibada ya Waislamu.
"Msikiti ni wakfu wa Kiislamu na mamlaka ya utawala huo haramu Israel hawana haki nayo," Al-Rajabi aliongeza kwa kusema; Aidha aliishutumu Israel kwa kutumia mzozo unaoendelea Huko Ukanda wa Gaza kuendeleza ajenda yao kwa kunyakua maeneo matakatifu yani ardhi zao.
Uvamizi wa utawala huo katili wa Israel Wafunga Msikiti wa Nabii Ibrahim (AS) kwa Waislamu Kuadhimisha Sikukuu za Kiyahudi.
Gavana wa Al-Khalil Khaled Dodin pia alilaani hatua hiyo ya kinyama na kuitaja kuwa ni shambulio "zito" dhidi ya alama za msikiti huo, uchochezi kwa Waislamu na shambulio dhidi ya uhuru wa kufanya Ibada.
Alionya kuwa jambo hilo linaweza kuzidisha hali ya wasiwasi katika eneo hilo.
Dodin alihimiza mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu na UNESCO kuchukua hatua za haraka kukomesha ukiukwaji huu haramu unaofanywa na Israel.
Msikiti wa Nabii Ibrahimi (AS) ambao uligawanywa kati ya waumini wa Kiislamu na Wayahudi kufuatia mauaji ya mwaka 1994 ya waumini 29 wa Kipalestina na Myahudi mwenye msimamo mkali Baruch Goldstein, mara kwa mara hufungwa kwa waumini wa Kiislamu na majeshi ya utawala huo haramu wa Israel ili kuruhusu walowezi kufanya sherehe za Kiyahudi.
Ndani ya Msikiti wa Nabii Ibrahimi (AS) huko Al-Khalil
Hebron ni nyumbani kwa takriban Waislamu 160,000 wa Kipalestina na walowezi wa Kiyahudi wapatao 500 wanaoishi katika maeneo yenye ulinzi mkali.